July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Albanie kurejesha viwanda Morogoro

Spread the love

MGOMBEA ubunge Jimbo la Morogoro Mjini Chadema, Marcossy Albanie amesema iwapo wananchi watamchagua, ndani ya miaka mitano ya uongozi wake atahakikisha anafufua viwanda ili kuchochea maendeleo mkoani humo. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Albanie amevitaja viwanda hivyo kuwa ni MOPROCO, TANNERIES, CARAMICS, CANVAS, POLYESTER, Magunia, Tumbaku, Moro Shoes, TANSEEDS, MORETCO, Mkonge Tungi, Mkonge Magereza, KOMOA na Mzinga Viazi.

Pia zipo kampuni za Mang’ula Mashine Tolls (MMT) na Karakana ya Reli Morogoro ambayo ndiyo karakana pekee yenye uwezo wa wa kufufua vichwa vya treni.

Akizungumza na MwanaHALISI Online leo asubuhi Albanie amesema “kufufua viwanda hivi, kutafufua uchumi wa Morogoro kwa faida ya wakulima, wafanyabiashara, wafanyakazi na jamii nzima kwa ujumla.”

“Viwanda hivi vitapunguza tatizo la ajira, kufufua biashara na huduma za jamii, kuongeza soko la mazao na kuongeza upatikanaji wa bidhaa,”amesema Albanie.

Aidha, Marcossy amevitaja vipaumbele vingine kuwa ni huduma bora za jamii (elimu, afya, maji na miundombinu mitaani), ajira siziso rasmi ikiwemo kilimo na biashara ndogondogo.

“Iwapo nitapewa ridhaa ya kuwa kiongozi wa jimbo hili pia nitahakikisha tunasimamia rasilimali za umma kwa maslahi ya Watanzania wote,” amesema Albanie.

error: Content is protected !!