August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Alan Pardew atimuliwa Crystal Palace

Alan Pardew

Spread the love

KLABU ya Crystal Palace ya nchini England imemtimua kocha wake Alan Pardew aliyekuwa akikinoa kikosi hicho baada ya kupoteza mechi nane kati ya michezo 10 katika ligi kuu nchini humo nakufanya klabu hiyo kushika nafasi ya 17 katika msimamo na kuwa katika hatari ya kushuka daraja.

Pardew ambaye alikuwa na msimu mzuri ndani ya klabu hiyo baada ya kuifanikisha kuingizaa kwenye fainali ya kombe la chama cha soka nchini humo (FA) mwezi Mei mwaka huu dhidi ya Manchester United na kupoteza mpambao huo baada ya kufungwa mabao 2-1.

Uwamuzi huo umekuja baada ya klabu hiyo kupoteza kwenye mchezo wake uliopita wa ligi dhidi ya Chelsea baada ya kukubali kufungwa bao mmoja kwa bila katika uwanja wao wa nyumbani na kutimiza idadi ya michezo nane bila kuona ushindi nakujikusanyia jumla ya pointi 15.

Mafanikio makubwa ya kocha huyo ni kufika fainali ya kombe la FA mara tatu, 1990 akiwa kama mchezaji ndani ya klabu hiyo, huku mwaka 2006 akiwa kocha wa West Ham United na 2016 akiiongoza tena Crystal Palace kama kocha lakini kote huko hakufanikiwa kutwaa taji hilo.

error: Content is protected !!