January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Al Shabab yaonesha jeuri yake Kenya

Spread the love

IKIWA ni siku mbili baada ya kuwepo kwa taarifa za mashambulizi ya kikundi cha kigaidi cha Al Shabaab cha Somali kuua wanajeshi wa Kenya, kundi hilo linaeleza kuwashikilia wanajeshi kadhaa wa Kenya.

Juzi kundi hilo lilivamia kambi ya jeshi iliyopo Kusini mwa Somalia na kusababisha mauaji ya wanajeshi zaidi ya 100 kutoka Muungano wa Afrika.

Leo kundi hilo limetoa taarifa kwamba, linawashikilia wanajeshi wa Kenya kama mateka kwenye maeneo yao ikiwa ni baada ya kushambulia kambi hiyo.

Baada ya mashambulizi hayo yaliyofanyika Ijumaa, Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta aliliambia taifa hilo kwamba, baadhi ya wanajeshi walio kwenye Jeshi la Muungano wa Afrika nchini Somalia waliuawa na wanamgambo wa Al Shabaab lakini hakueleza idadi ya vifo hivyo.

Kiongozi wa kundi hilo kwenye mashambulizi hayo Saleh Ali Saleh Nabhan alikuwa kiongozi wa kundi la al Qaeda katika eneo la Afrika Mashariki ambaye aliuawa katika shambulio la Marekani nchini Somalia mwaka 2009.

Al Shabaab wamekuwa wakitekeleza mashambulizi ya mara kwa mara nchini Kenya na Uganda. Kundi hilo limekuwa likitoa wito kwa Kenya kuondoa wanajeshi wake Somalia na wasipofanya hivyo wataendelea kufanya mashambulizi hayo ndani na nje ya Kenya.

error: Content is protected !!