WANAMGAMBO wa kundi la Al shabab wanatajwa kuchinja watoto kadhaa katika Mkoa wa Cabo Delgado, nchini Msumbiji. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Taarifa hiyo imetolewa na Shirika la Save the Children, jana Jumatatu tarehe 15 Februari 2021, ni baada ya shirikia hilo kuzungumza na walioathiriwa na matukio hayo wiki iliyopita.
Kwa mujibu shirika hilo, baadhi ya wananchi wamelazimika kukimbia makazi yao na kwenda katika vijiji jirani kutafuta hifadhi.
Hadi sasa inakadiriwa zaidi ya watu 2,500 wameuawa na wanamgambo hao, huku wengine 700,000 wakitoroka tangu mkoa huo wa Cabo Delgado ulioko Kaskazini mwa Msumbiji, kuvamiwa mwaka 2017.
Hivi karibuni, Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi alimfukuza kazi Mkuu wa Jeshi la Ardhini nchini humo, Ezequiel Isac Muianga na Mkuu wa Jeshi la Anga Anga, Messias Andre Niposso.
Vilevile, alimfukuza kazi Kamanda wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Marechal Samora Macheya. Hatua hiyo ilihusishwa na viongozi wa vikosi hivyo kushindwa kudhibiti wanamgambo hao.
Leave a comment