May 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Al Merreikh wamtengea Manula donge nono

Spread the love

 

KLABU ya Al Merreikh inayoshiki Ligi Kuu nchini Sudan imeonekana kutaka saini ya mlinda mlango wa klabu ya Simba na Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Aisha Manula kiasi cha kutenga shilingi milioni 18.5 kama mshahara kwa mwezi. Anaripoti Mwandishi Wetu

Manula ambaye kwa sasa ni moja ya walinda mlango hodari ndani ya bara la Afrika kiasi cha kuwa kati ya magolikipa waliokoa mpira mingi ya hatari (Saves) kwenye michuano ya Chan iliyofanyika Januari 2021, nchini Cameroon.

Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali nchini Sudan zinaeleza kuwa mabosi wa klabu hiyo wapo tayari kulipa kiasi cha dola za kimarekani 100,000 sawa na fedha ya kitanzania shilingi 231,635,000 milioni kama pesa ya usajili.

Matajili hao wa sudan wamevutiwa na mlinda mlango huyo kutokana na rekodi nzuri aliyekuwa nato sasa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika hatua hii ya makundi.

Al Merreikh kwa sasa wapo kwenye mchakato wa kutengeneza kikosi chao na kupelekea kufanya mabadiliko kwenye benchi lao la ufundi kwa kumtimua aliyekuwa kocha wao Nasreddline Nabipamoja na msaidizi wakemara baada ya sare ya bila kufungana dhidi ya Simba.

Mpaka sasa Manula amecheza jumla ya dakika 270, kwenye hatua ya makundi klabu bingwa barani Afrika sawa na michezo mitatu ambao hajaruhusu bao lolote kupita akiwa kwenye milingoti mitatu.

Mchezo pekee alioukosa Manura kwenye klabu bingwa ulikuwa dhidi ya Al Merreikh ugenini kutokana na kupata madhira kwenye mchezo wa Ligi dhidi ya Jkt Tanzania mara baada ya kugongana na mshambuliaji Dany Lyanga na kupoteza fahamu.

Manula ambaye alijiunga ndani ya klabu ya Simba 2017 na kufanikisha timu hiyo kutwaa mataji matatu ya ligi Kuu Tanzania Bara na kufika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu wa 2018/19.

Mlinda mlango huyo aliyekuwa kwenye kiwango bora kwa sasa ndani nan je ya Tanzania alifanikiwa kuchukua tuzo ya golikipa bora kwenye msimu wa ligi uliomalizika.

Kwa sasa Manula bado ni mchezaji wa Simba huku mkataba wake ukisalia miezi mitatu, mara baada 11 Juni 2019 kusaini mkataba wa miaka mitatu.

 

 

error: Content is protected !!