Thursday , 25 April 2024
Home Kitengo Michezo Al Ahly yampa noti Miquissone
Michezo

Al Ahly yampa noti Miquissone

Spread the love

 

KIUNGO mshambuliaji wa klabu ya Simba, Luis Miquissone amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Februari 2021 wa klabu hiyo na kukabidhiwa fedha Shilingi milioni moja kutoka kwa wadhamini wa tuzo hizo, Kampuni ya Emirates Aluminium Profile. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezaji huyo amekabidhiwa kiasi hiko cha fedha hii leo tarehe 17 Machi 2021, jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari sambamba na tuzo.

Miquisone ameshinda tuzo hiyo mara baada ya kuibuka mchezaji bora kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ambao uliomalizika kwa Simba kushinda bao 1-0.

Mchezo huo wa kundi A, ulifanyika jijini Dar es Salaam tarehe 23 Februari 2021, kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa ambapo bao pekee la Simba lilifungwa na Luis Miquissone.

Mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo Miquison alisema: “Nataka kuwashukuru kwa tuzo hii, lakini tuzo hii sio ya kwangu bali ni kwa timu nzima.”

Mara baada ya kumaliza mchezo dhidi ya Al Ahly mchezaji huyo alichaguliwa na Shirikisho la Mpira Miguu Afrika (Caf) kuingia kwenye kikosi cha wachezaji 11 wa wiki.

Miquissone ameshinda tuzo hiyo mara baada ya kumbwaga mchezaji mwenzie Joash Onyango, raia wa Kenya anayecheza kwenye nafasi ya beki wa kati.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!