Tuesday , 30 May 2023
Home Kitengo Michezo Al Ahly kuiponza Yanga
Michezo

Al Ahly kuiponza Yanga

Spread the love

BAADA ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Al Ahly kwenye mchezo wa Klabu Bingwa barani Afrika hatua ya makundi, Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba, Patrick Aussems amesema kuwa, kwa sasa nguvu zote wanazielekeza kwenye mchezo dhidi ya Yanga. Anaripoti Kelvin Mwaipungu… (endelea).

Kocha huyo alieleza hayo mara baada ya mchezo kumalizika na kusema, kwa sasa hawatazami michezo ya klabu bingwa kwa kuwa, wanawiki tatu za maandalizi na kwamba, Mechi yao dhidi ya yanga ndio uliopo karibu.

“Tunakutana na Yanga kwenye mchezo siku ya Jumamosi ila kwa sasa acha tufurahie ushindi, tutarudi kambini kwa sababu tunacheza Jumamosi na kesho tutaanza maandalizi kuelekea mchezo huo,” alisema Aussems.

Kwa ushindi huo, kikosi cha Simba kinaonekana kuwa na hali nzuri kuelekea mchezo dhidi ya wapinzani wao wa kubwa kihistoria na kwenye Ligi Kuu msimu huu kwa kuwa, ndio walipewa nafasi kubwa kutwaa ubingwa huo.

Kuelekea mchezo huo, Yanga imejichimbia mkoani Morogoro kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo ambao utakuwa na umuhimu mkubwa kwa kila timu.

Mchezo huo ambao utakuwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara unatarajia kuchezwa siku ya Jumamosi wiki hii majira ya saa 11 jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

NBC Dodoma Marathon yazinduliwa, wakiambiaji 6,000 kushiriki

Spread the loveBENKI ya NBC imetangaza kufanyika kwa mbio kubwa za NBC...

Michezo

Rais Samia anunua tiketi 5000 Yanga vs USM Alger

Spread the loveRAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu...

Michezo

Mwenyekiti UVCCM anogesha nusu fainali Kimwanga CUP, Hawa Abdul Rede CUP kwa kishindo

Spread the loveHEKAHEKA za michuano ya kuwania kuingia fainali ya michuano ya...

Michezo

Yanga SC. yatwaa ubingwa wa pili mfululizo

Spread the love  KLABU ya Yanga SC imeweka rekodi ya kutwaa ubingwa...

error: Content is protected !!