July 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Akutwa na SMG, risasi 30

Spread the love

GODFREY Octavian (44), Mkazi wa Mkundi, Morogoro anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo kwa tuhuma za kukutwa na bunduki aina ya Sub Machine Gun (SMG), anaandika Christina Haule.

Octavian alikuwa ameifukia ardhini bunduki hiyo jirani na nyumba yake huku akiizungushia mkeka na pembeni yake kukiwa na magazine moja yenye risasi 30.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana Ulrich Matei, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro amesema kuwa, mtuhumiwa alikamatwa  Septemba 13 mwaka huu saa 3:00  usiku katika maeneo ya Mlima Mzembe uliopo Kata ya Mkundi, Manispaa ya Morogoro.

Kamanda huyo amesema kuwa, polisi wakiwa katika harakati za kupambana na uhalifu wa kutumia silaha, walimkamata mtuhumiwa huyo akiwa na silaha hiyo pamoja na risasi zingine 39 alizohifadhi kwenye mfuko wa plastiki pamoja na risasi mbili za bunduki aina ya Rifle.

Matei amesema kuwa, baada ya polisi kufanya upekuzi nyumbani kwake, walifanikiwa kupata magazine na risasi hizo kisha kwenda kuonesha mahali alipoficha silaha hiyo.

Kamanda Matei amesema kuwa, uchunguzi zaidi unaendelea na mtuhumiwa atafikishwa mahakani pindi uepelelezi utakapokamilika.

 

 

 

error: Content is protected !!