January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ajira ya mahakimu zakosa waombaji

Mahakama ya Mwanzo, Kinampanda wilayani Iramba katika Mkoa wa Singida

Spread the love

SERIKALI imesema kuwa kati ya nafasi za mahakimu 300 zilizotangazwa, ni watano pekee walioomba na kuajiriwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2014/15. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima, ameliambia Bunge kuwa, fedha kwa ajili ya kuwaajiri mahakimu 300 zilikwepo.

Malima amesema mpango wa kuajiri wengine 295 bado upo palepale na kwamba wanatarajia kufanya hivyo katika kipindi cha mwaka huu wa bajeti 2015/16.

Malima akijibu swali la la nyongeza la mbunge wa Lushoto, Henry Shekifu (CCM), ambaye alitaka kujua ni kwa nini kuna upungufu wa mahakimu nchini wakati kuna chuo kinachofundisha kada hiyo cha Lushoto mkoani Tanga.

Awali katika swali la msingi la mbunge wa Viti Maalum, Sabreena Sungura (Chadema), alitaka kujua seikali ina mkakati gani wa kupunguza kero za wananchi kuhusu kulipa maduhuli ya serikali kwa benki ya NMB hata kwa kiwango cha Sh. 1500 wakati maeneo mengine yako mbali na benki.

Naibu Waziri, alikiri Mahakama kuanza kukusanya maduhuli kwa njia ya kulipia benki lengo likiwa ni kupunguza malalamiko mbalimbali ya wateja hususani yanayohusiana na rushwa pamoja na kudhibiti upotevu wa maduhuli ya Serikali.

“Serikali iliamua kutumia benki ya NMB kwa sababu ndiyo benki pekee yenye mtandao mpana wa matawi kwenye wilaya zote nchini, hata hivyo, mahakama ya Tanzania inaendeleo kufanyia tathmini changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa utaratibu huu,” amesema.

Malima amesema kwa kutambua usumbufu wanaoupata baadhi ya wananchi kutokana na kuwa mbali na huduma za kibenki, tayari NMB wameanza kufanya tahimni ili kuona kama kutakuwa na uwezo wa kulipia huduma kupitia mitandao ya simu.

error: Content is protected !!