November 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ajira ualimu kizungumkuti, 89,958 wajitosa, nafasi ni 6,949

Waziri wa Nchi Ofisi a Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Ummy Mwalimu

Spread the love

 

WAZIRI wa Ofisi ya Rais-Tamisemi, Ummy Mwalimu, amekiri uwepo wa tatizo la ukosefu wa ajira za ualimu nchini, akisema kwamba, nafasi zinazotolewa serikalini hazikidhi mahitaji ya waombaji. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Ummy amesema hayo leo Jumanne tarehe 25 Mei 2021, bungeni jijini Dodoma, akimjibu Mbunge wa Longido (CCM), Dk. Stephen Kiruswa, aliyeiomba Serikali iwape kipaumbele waalimu wanaojitolea, inapoajiri watumishi wapya.

Ummy amesema kuna wahitimu wa vyuo vya ualimu kuanzia mwaka 2012 hadi 2015, bado hawajapa ajira na kwamba Serikali huwapa kipaumbele, inapotangaza nafasi za ajira.

“Kuna waalimu wamemaliza 2012, 2013, 2014 na 2015 hawajaajiriwa, lakini upo mtizamo ndani ya wizara labda tuangalie hawa ambao wamemaliza siku nyingi, wamejitolea na hawajapata ajira. Kwa sababu muda wao wa kuajiriwa serikalini unapungua. Lazima wajairiwe kabla ya miaka 45,” amesema Ummy.

Akielezea changamoto hiyo, Ummy amesema katika tangazo la nafasi za ajira 6,949 za ualimu, zilizotangazwa hivi karibuni na Serikali, hadi kufikia juzi tarehe 23 Mei 2021, watu 89,958 wamejitokeza kuomba nafasi hizo.

“Suala hili ni tete, nafasi ni 6,949 lakini mpaka juzi walioomba wameshafika 89,958. Kwa hiyo katika suala hili naomba mtuamini, Serikali tutatenda haki. Hata hao wanaojitolea tutawatambua, kama kweli wanajitolea,” amesema Ummy.

error: Content is protected !!