May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ajira milioni 12.7 zazalishwa Tanzania

Baadhi ya vijana waliojitokeza kwenye usaili wa ajira za Uhamiaji

Baadhi ya vijana waliojitokeza kwenye usaili wa ajira za Uhamiaji

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, imsema jumla ya ajira zaidi ya milioni 12.77 zimezalishwa katika kipindi cha kuanzia mwaka 2017 – 2020, ikiwa ajira za moja kwa moja milioni 11.89 na zisizo rasmi 881,354. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ni kauli ya Dk. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango aliyoitoa leo Alhamisi tarehe 7 Aprili 2021, bungeni jijini Dodoma, wakati akiwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa kwa miaka mitano (2021/22 – 2025/26).

“Jumla ya vijana 65,008 katika kipindi cha mwaka 2017 hadi 2020, wamepatiwa mafunzo ya ujuzi na stadi za kazi ikiwemo mafunzo ya uanagenzi katika fani za ujenzi, useremala, umeme wa majumbani na viwandani, umeme wa jua, ufundi magari.”

“Pia, ufundi bomba, utengenezaji wa vifaa vya aluminium, uchomeleaji na uungaji vyuma, kilimo na ufugaji, ushonaji, uchorongaji vipuli, uchapaji nyaraka na TEHAMA,” amesema.

Dk. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango

Akiwasilisha mpango huo, Dk. Mwigulu amesema, serikali imeendelea kulinda ajira za wazawa kwa kuhakikisha, kuwa wageni wanaokuja kufanya kazi nchini, wanakidhi vigezo vilivyoainishwa katika Sheria ya Kuratibu Ajira za Wageni Na. 1 ya mwaka 2015.

Amesema, shabaha za mpango huo wa tatu ni pamoja na kuongeza kiwango cha ukuaji wa uchumi kwa mwaka kutoka asilimia 6.0 mwaka 2021 na kufikia wastani wa asilimia 8.0 ifikapo mwaka 2026.

“Mapato ya ndani ikijumuisha mapato ya halmashauri kuongezeka kutoka asilimia 15.9 ya Pato la Taifa mwaka 2021/22 hadi asilimia 16.8 mwaka 2025/26.

“Mfumuko wa bei kuendelea kubaki katika wigo wa tarakimu moja ya wastani wa asilimia kati ya 3.0 – 5.0 katika kipindi cha muda wa kati,” amesema.

Pia, amesema, mpango huo unalenga akiba ya fedha za kigeni kukidhi mahitaji ya uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje kwa kipindi kisichopungua miezi minne.

Amesema, anatarajia sekta binafsi kuzalisha ajira mpya zipatazo milioni nane kati ya Julai 2021 na Juni 2026.

Dk. Mwigulu amesema, ili mpangpo huo kutimia, unakadiriwa kugharimu jumla ya sh. 114.8 trilioni zikijumuisha mchango wa sekta binafsi wa sh. 40.6 trilioni na sekta ya umma sh. 74.2 trilioni kutoka vyanzo vya mapato ya kodi na yasiyo ya kodi, misaada na mikopo.

error: Content is protected !!