August 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ajira 736 kutangazwa upya baada ya kukosekana waombaji wenye sifa

Spread the love

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Innocent Bashungwa amesema nafasi 736 kada za afya zimekosa waombaji wenye sifa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Bashungwa ametoa kauli hiyo leo tarehe 26 Juni, 2022 wakati akitangaza majina 16,676 ya watumishi wapya waliopangiwa vituo vya kazi katika Sekta ya Elimu na Afya nchini.

Orodha hiyo inatokana na waombaji wenye sifa waliokidhi vigezo baada ya Aprili, 2022 Rais Samia Suluhu Hassan kutoa kibali cha ajira kwa kada za Ualimu na Afya, kwa ajili ya kuajiri walimu 9,800 wa shule za msingi na sekondari na wataalam wa afya 7,612.

Amesema, baada ya kupata kibali cha ajira, Ofisi ya Rais-TAMISEMI ilitoa tangazo kwa wahitimu mbalimbali wa Ualimu na Kada za Afya, kuwasilisha maombi ya kazi, kupitia mfumo wa kielektroniki wa kupokea na kuchakata maombi ya ajira, kuanzia tarehe 20 Aprili hadi 8 Mei, 2022.

Amesema, jumla ya maombi 165,948 yakiwemo ya wanawake 70,780 na wanaume 95,168 yaliyopokelewa kwenye mfumo, ambapo maombi ya kada za afya ni 42,558, na kada ya Ualimu ni 123,390.

Amesema kada zilizokosa nafasi ni Daktari wa Meno (50), Tabibu Meno (43), Tabibu Msaidizi (244), Mteknolojia Mionzi (86) na Muuguzi ngazi ya cheti (313).

Waziri amesema, kada hizi zitarudiwa kutangazwa ili kupata waombaji wenye sifa watakaojaza nafasi.

error: Content is protected !!