May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ajifungua watoto tisa kwa mpigo

Spread the love

 

HALIMA Cisse (25), raia wa Mali, Magharibi mwa Afrika, ameibua gumzo nchini mwake na katika mitandao ya kijamii baada ya kujifungua watoto tisa. Inaripoti mitandao ya kimataifa…(endelea).

Mwanamke huyo, amejaaliwa watoto hao jana Jumanne tarehe 4 Mei 2021, ambapo wanne kati ya watoto hao ni wavulana.

Halima amejifungua watoto akiwa katika hospitali moja nchini Morocco alikokuwa amelazwa. Mwanamama huyo alijifungua kwa njia ya upasuaji.

Taarifa za hospitali hiyo zimeeleza, kutokana na uchunguzi wa awali katika hospitali ya Mali na Morocco aliko sasa ulionesha, Halima alitarajiwa kujifungua watoto saba.

Hata hivyo, hospitali hiyo ya Morocco imeeleza, Halima na wanawe wote wanaendelea vizuri na wana afya njema. Na kwamba, anatarajiwa kurejea nyumbani kwao (Mali) wiki chache zijazo.

error: Content is protected !!