September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ajali yaua 19 Iringa, Rais Samia awalilia

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametuma salama za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Qeen Sendiga kufuatia ajali ya barabara iliyoua watu 19 na baadhi wakijeruhiwa. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Ajali hiyo imehusisha basi dogo la abiria aina ya Coaster na lori la mizigo iliyotokea eneo la Changarawe, Mufindi mkoani Iringa alfajiri ya leo Ijumaa, tarehe 10 Juni 2022.

Kati ya waliofariki, 14 ni wanaume, wanne ni wanawake na mtoto mmoja.

Taarifa ya Zuhura Yunus, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu imesema, Rais Samia amevitaka vyombo vyote vinavyosimamia usalama barabarani kuendelea kutoa elimu kwa madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani.

error: Content is protected !!