December 4, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ajali ya treni yajeruhi watu tisa

Spread the love

WATU tisa wamejeruhiwa katika ajali ya treni iliyotokea asubuhi ya leo tarehe 2 Novemba 2018 maeneo ya Karakata wilayani Ilala jijini Dar es Salaam. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Taarifa ya ajali hiyo imethibitishwa na Kamanda wa Reli nchini, David Mnyambugha akisema kuwa majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa hospitalini kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa Mnyambugha, ajali hiyo pia imesababisha kuharibika vibaya kwa mabehewa mawili.

Katika hatua nyingine, amesema mabehewa hayo hayafai kuendelea na safari hadi yavutwe, na kwamba taarifa kuhusu safari za treni hiyo itatolewa hapo baadae na mamlaka husika ambayo ni Shirika la Reli nchini (TRC)

error: Content is protected !!