August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ajali ya basi Dar, mmoja ateketea kwa moto

Basi la Al Saed na Roli yakiendelea kuteketea kwa moto

Spread the love

Habari zilizotufikia hivi punde, zinasema ajali mbaya ya kati ya basi la abiria liitwalo Safari Njema lenye namba ya usajili T 990 AQF na lori lenye namba ya usajili 534 BYJ na kusababisha kuwaka kwa magari hayo yote mawili na kupelekea kifo cha abiria mmoja na majeruhi 10, Anaandika Charles William.

Ajali hiyo imetokea mcahana wa leo katika eneo la Kimara stop over, Ubungo jijini Dar es Salaam.

“Lori lilikuwa limebeba mifuko ya saruji likielekea Mbezi na lilikuwa kwenya kasi kubwa na magari ya mbele yake yalipofunga breki za ghafla ikabidi lori hilo liyakwepe na kukutana uso kwa uso na basi hilo.

 

Magari yote mawili yameungua na tumeshuhudia mwili ulioteketea kwa moto,” ameeleza shuhuda wetu.

Taarifa kamili itatolewa baada ya mamlaka mbalimbali  likiwemo Jeshi la Polisi kutoa taarifa rasmi.

error: Content is protected !!