July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ajali mbaya Dar es Salaam

Spread the love

AJALI mbaya imetokea leo asubuhi katika Barabara ya Mandela, eneo la Matumbi jijini Dar es Salaam ikihusisha lori lililokuwa limebeba ng’ombe na daladala ina ya DCM lililokuwa limebeba abiria, anaandika Faki Sosi.

Katika ajali hiyo, watu kadhaa wamepoteza maisha huku ng’ombe pia wakiripotiwa kufa. Mashuhuda wa ajali hiyo wameeleza kuwa, lori hilo limevamia daladala hiyo na kusababisha mauaji hayo.

Magari hayo mawili yameharibika vibaya huku ajali hiyo ikisababisha foleni kubwa kwenye barabara hiyo. Taratibu mbalimbali kuhusu ajali hiyo zinaendelea kufanyika.

Taarifa zaidi zitakujia hivi punde…

error: Content is protected !!