August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ajali Karatu, wanafunzi 32 wathibitishwa kupoteza maisha

Picha za ajali hiyo

Spread the love

KAMANDA wa Polisi, mkoani Arusha, Charles Mkumbo amethibitisha kuwa watu 32 wamefariki katika ajali iliyotokea wilayani Karatu, eneo la Rhotia Marera, anaandika Hamisi Mguta.

Waliofariki katika ajali hiyo ni wanafunzi 29 wa darasa la saba mchepuo wa kingereza katika shule ya msingi Lucky Vincent mkoani humo na walimu wawili pamoja na Dereva wa gari hilo ambao walikuwa wakielekea shule iitwayo Tumaini kwa ya kufanya mtihani wa ujirani mwema.

Miongoni mwa wanafunzi waliofariki ni pamoja na wavulana 11 na wasichana 18 ambao maiti zao zimepelekwa katika hospitali ya Lutheran Karatu.

Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi

Kufiatia tukio hilo Rais Magufuli ametuma saalamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa huo, Bw. Mrisho Gambo na kueleza kuwa ajali hiyo imezima ndoto za watoto waliokuwa wakijiandaa kulitumikia taifa.

“Ndugu. Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo naomba unifikishie pole nyingi kwa wazazi, ndugu, jamaa na marafiki wote wa wanafunzi, walimu na dereva waliopoteza maisha. hiki ni kipindi kigumu kwetu sote na uwaambie naungana nao katika majonzi na maombi.

“Muhumi kwa sasa tuwaombee marehemu wote wapunzike mahala pema, majeruhi wapone haraka na wote walioguswa na msiba huu wawe na moyo wa subir, ustahamilivu na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu” amesema kupitia taarifa yake.

error: Content is protected !!