August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Aibu matokeo Kidato cha Nne yaizindua Morogoro

Spread the love

AIBU ya matokeo mabaya ya Mtihani wa Kidato cha Nne uliofanyika mwaka jana, imeizindua Sekta ya Elimu wilayani Malinyi, Morogoro, anaandika Christina Haule.

Malinyi imeamua kuweka mkakati wa kuinua kiwango cha taaluma ili kuepukana fedheha waliyopata ya kuwa na shule tatu kati ya 10 zilizofanya ovyo kwenye mtihani huo nchini.

Dk. Khaji Mponda, Mbunge wa Jimbo la Malinyi wilayani Malinyi amesema hayo leo wakati akizugumza na waandishi wa habari.

Amesema kuwa, amepokea kwa masikitiko taarifa za kufeli kwa wanafunzi kwenye shule tatu wilayani humo ambapo wameshaanza kuweka mikakati ya kunusuru suala la elimu wilayani humo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wazazi wanashirikiana na walimu kukagua kazi za wanafunzi.

Dk. Mponda amesema kuwa, watahakikisha wanaendelea kutoa chakula kwa wanafunzi ambapo ameiomba serikali kupeleka walimu wa masomo ya kisayansi.

Amesema wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto ya mfumo mbovu wa usajili wa wanafunzi wa Kidato cha Kwanza ambapo hufikia wakati baada ya usaili hubaini kuwepo kwa wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika.

Anslem Mponji, Mwalimu wa Shule ya Malinyi ameiomba serikali kuhakikisha inajenga nyumba za walimu karibu na maeneo ya shule jambo litakalofanya wanafunzi wanaotoka umbali mrefu kubaki shuleni kufundishwa masomo ya ziada na walimu wao.

James Nicodem, Ofisa Elimu Taaluma Wilaya amesema kuwa, wilaya hiyo inakabiliwa na upungfu wa walimu hasa wa masomo ya sayansi licha ya serikali kuweka mkakati wa kupeleka walimu kila wilaya na kwa kila mwaka.

error: Content is protected !!