January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ahadi za Kikwete zaitesa Bunge la 11

Spread the love

AHADI za Rais Jakaya Kikwete bado zinaendelea kulitesa bunge la 11 ambalo liko chini ya utawala wa Rais Dk John Magufuli na wabunge wanaendelea kuhoji utekelezaji wake. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Wabunge wanahoji utekezaji wa ahadi hizo utafanyika lini kwani ziliahidiwa kwa muda mrefu lakini kasi ya utekezaji wake unakwenda kwa kusuasua.

Mbunge wa Sumve (CCM) Richard Ndasa alitaka kujua ujenzi wa barabara kwa kinwago cha lami kutoka Magu –Bukwimba – Ngudu –Hungulamwa ambayo ilikuwa ni ahadi ya siku nyingi katika utawala wa serikali ya awamu ya nne.

“Mheshimiwa Spika, nilitaka kujua ujenzi huo utakamilika lini kwani ni ahadi ya serikali ya awamu ya nne na wakati Rais Kikwete akiahidi na Rais Magufuli alikuwepo wakati huo akiwa Waziri wa Ujenzi,” amesema Ndasa.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani amesema kuwa Serikali imekuwa ikifanya kila jitihada kwa ajili ya kutekeleza ahadi zote ambazo zimeahidiwa lakini ufinyu wa bajeti ndiyo changamoto.

Naibu Waziri amesema katika kipindi vcha 2010/11, Wizara kupitia kwa wakala wa barabara Tanrods ilitenga kiasi cha Sh 1.2 bilioni ambazo zilitumika kwa ajili ya ujenzi wa kiwango cha lami barabara Magu – Ngudu – Jojiro.

Amesema ujenzi huo ni wa sehemu ya Ngudu Mjini yenye urefu wa kilomita 1.9 ambazo amesema ni moja wapo ya juhudi katika kukalimisha ahadi hiyo.

Ngonyani amesema kwa mwaka 2014/15 na 2015/16, Serikali ilitenga jumla ya Sh. 200 milioni kwa ajili ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 70.

Kwa mujibu wa Ngonyani, taratibu za kumtafuta mhandisi mshauri zinaendelea na baada ya kukamilika kwa usanifu na gharama za mradi huo kujulikana, serikali itatafuta fedha za kuanza ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami.

error: Content is protected !!