Saturday , 9 December 2023
Habari za SiasaTangulizi

Ahadi ya Chadema 2020

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeweka ahadi ya kutovumilia kunyongwa kwa haki, kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu. Anaripoti Regina Monde, Dar es Salaam …(endelea).

John Mnyika, Katibu Mkuu Chadema ametoa kauli hiyo leo tarehe 29 Januari 2020, wakati akihojiwa katika kipindi cha Konani, kinachorushwa na mtandao wa ITV.

Amesema, kama Tume Huru ya Uchaguzi haitapatikana na au mchakato wa uchaguzi huo utagubikwa na dalili za uvunjifu wa sheria na Katiba, watawaelekeza wanachama wao kuchukua hatua, kabla ya uchaguzi huo kufanyika.

“Tudai Tume Huru, kama isipopatikana tutawaelekeza Watanzania nini cha kufanya kabla ya uchaguzi kufika. Tuyapate mabadiliko na uhuru wa kweli bila kujali kuna Tume Huru ama hakuna Tume Huru,”ameeleza Mnyika.

Mnyika amesema, Chadema ilitumia busara katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2019, kwa kuwadhibiti wafuasi wake kuchukua hatua juu ya ukiukwaji wa sheria na kanuni za uchaguzi, uliofanyika katika mchakato wa uchaguzi huo.

“Ninachokiona mimi kwa kilichotokea uchaguzi wa serikali za mitaa, ninyi mliokuwa na uamuzi wa kuwaambia Watanzania, kwa kusema hatutabariki udhalimu huu.

“Lakini tukanyamza kimya kuruhusu watu wetu kuchukua uamuzi unaofaa, kama tungeruhusu sasa hivi ingekuwa mengine, sasa tunachowaambia watawala, tumechoka kuwatuliza watu wetu,” amesema Mnyika na kuongeza;

“Tunaamini amani ni tunda la haki, tumeishajifunza kilichotokea. Uchaguzi 2020 tunaiambia serikali mambo mawili, iufute uchaguzi wa serikali za mitaa. Hatuhesabu ni uchaguzi, tunaona ni uchafuzi ndio maana tukaagiza wanachama wasitambue viongozi, umeacha mpasuko.”

Aidha, Mnyika ametoa wito kwa wafuasi wa Chadema na Watanzania kwa ujumla kuhakikisha, wanarudisha umoja na mshikamano wa nchi, uliasisiwa na Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

“Taifa lililounganishwa kwa makabila tofauti, linapasuka kwa ubaguzi wa kisiasa. Huyu chama hiki na  huyu kile, watawala wanakemea watu wanaochagua upinzani, wanawaambia kawaambie wapinzani wakupe maji wakati yanapatikana kwa kodi zao.

“Suluhisho sisi wananchi tuungane, tuseme imetosha kwa umoja wetu tutumie uchaguzi 2020 kupitia kura. Huu ndio mwaka wa kuleta mabadiliko ya kweli ili tupate uhuru wa kweli,” amesema.

Ametoa mfano wa Zanzibar kwamba, haikufanya mapinduzi ili kupeperusha bendera, “hatujapata uhuru ili kupeperusha bendera, wala Zanzibar hawakufanya mapinduzi ili wasimamishe bendera, bali walitaka uhuru wa watu ambao nyenzo ya kuleta maendeleo ya watu.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Miaka 62 ya uhuru tujenge upya mioyo yetu

Spread the loveWAKATI Tanganyika ikiadhimisha miaka 62 tangu kupata uhuru, Mwenyekiti wa...

Habari za Siasa

Rais Samia asamehe wafungwa 2,244

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewasamehe wafungwa 2,244, huku akiwabadilishia...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataka jamii inayohoji mafisadi

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan ametoa maagizo juu ya uboreshaji dira...

Habari za SiasaTangulizi

Kapinga: Kukatika kwa umeme siyo hujuma

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema Serikali ipo kazini...

error: Content is protected !!