June 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Agosti 29 Lowassa Jangwani

Spread the love

KAIMU Katibu Mkuu Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Salim Mwalim amewatangazia wananchi kuwa, Agosti 29 mwaka huu chama hicho kitazindua kampeni. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Mwalimu amesema Lowassa na mgombea mwenza wake Juma Duni Hajji ambao pia ni wawakilishi wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wanatarajia kuanza rasmi kampeni hizo kuelekea Uchaguzi Mkuu 25 Oktoba mwaka huu.

Vyamavinavyounda UKAWA ni Chadema yenyewe, Chama cha Wananchi (CUF), Chama cha NCCR-Mageuzi pamoja na NLD.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Chadema leo Jijini Dar es Salaam, Mwalim amesema awali kampeni hizo zilitarajiwa kuzinduliwa 25 Agosti katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam lakini serikali ilizuia.

Akieleza sababu za kutaka uzinduzi huo ufanyike Uwanja wa Taifa, Mwalim ameeleza kuwa ni kutokana na usalama wa wananchi na idadi kubwa ya watu waliotarajiwa kuhudhulia katika mkutano huo.

“Hizo ndizo zilikuwa sababu zetu na si vinginevyo. Sababu zilizotolewa na serikali yetu hazina nguvu kwa kile walichokidai uwanja ule hauwezi kutumika kwa mihemuko ya kisiasa.

“Tulisikitishwa sana na hawa wenzetu kutunyima sisi uwanja kwa kigezo cha kuharibu wakati mpira unachezeka humo humo hawaogopi kuharibiwa.” Amesema Mwalim.

Aidha, ametoa wito kwa wanachama wa UKAWA kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili kusikiliza sera za ukombozi kwa wananchi.

Mbali na hilo, Mwalim amezungumzia kuhusu taarifa zilizotolewa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwamba wameshinda majimbo yote matano sio kweli na kwamba, majimbo hayo yote yamewekewa pingamizi.

Amesema, tayari waogombea wa majimbo hayo wamekata rufaa kwenda Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), hivyo inasubiriwa hukumu.

Akitaja majimbo hayo ambayo yamekatiwa rufaa kuwa ni Bumbuli, Mlalo, Handeni Mjini, Peramiho, Ludewa na Chalinze.

Amesema, katika majimbo hayo yote wanachama wa Chadema walionekana kuonewa tofauti na wagombea wa CCM.

Pia, ameitaka (NEC) kufuata misingi bora ya uchaguzi pasipokutoa upendeleo kwa chama kimoja.

“Tunashidwa kuelewa maamuzi yao yanavyotolewa na kama wanafanya kazi kwa ajili ya CCM waseme tu ili tuwaachie kuliko kufanya dhuluma maana haiwezekani makosa makubwa wanayaacha ila ya kwetu madogo wanayashikilia.

“Wananchi wasiwe na wasiwasi, kila kitu kitakuwa sawa. Kama sheria inafuata mkondo basi kila kitu kitakuwa sawa kwani tayari kuna wanasheria wetu wanalishughulikia.”

error: Content is protected !!