Friday , 1 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Agnesta awaongoza wanaume Segerea
Habari za Siasa

Agnesta awaongoza wanaume Segerea

Agnesta Lambert, Mgombea Ubunge Jimbo la Segerea (Chadema)
Spread the love

AGNESTA Lambert, Mratibu wa Uhamasishaji wa Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bawacha) ameshinda kura za maoni za mgombea ubunge Segerea. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam…(endelea).

Katika kura za maori zilizofanyika leo tarehe 13 Julia 2020 Lambert ameshinda kwa kupata kura 76 kati ya 144.

Agnesta amewashinda John Mrema, mkurugenzi wa itifaki, mawasiliano na mambo ya nje wa chama hicho aliyepata kura 56, Masato Wasira kura 7, Gango Kidela kura 3 na Andrew Kimbombo aliyepata kura 1 na kura moja imeharibika.

Akizungumza mara baada ya ushindi huo, Agnesta amesema, ameupokea kwa furaha ushindi huo licha ya kuwa bado anasubiri maamuzi ya Kamati Kuu ya chama itakayopitisha rasmi wagombema wote wa ubunge.

“Nakosa maneno ya kusema kwasababu nilikuwa kwenye kinyang’anyiro ambacho nilikuwa na wanaume na nafahamu ilikuwa mchakato wa awali na kuna mchakato mwingine unakuja kwa ajili ya Kamati Kuu kumpitisha mgombea,” amesema

“Siri ya ushindi huu ni namna ambavyo ninaishi na wanachama wenzangu vizuri pamoja na viongozi wangu na kuwa mfano mzuri kwao katika ujenzi wa chama”.

Alipoulizwa Kama jina lake halitapitishwa na Kamati Kuu kwa jailli ya kuwa mgombea kuwakilisha chama ngazi ya jimbo, amesema itakuwa ni furaha kwake hata kama hatachaguliwa kugombea kwakuwa hata atakayewekwa atakuwa mwanachadema.

“Nipo tayari kupokea mabadiliko yoyote lakini pia nipo tayari kuipeperusha bendera ya chama ngazi ya jimbo kwasababu niliamua kuomba ridhaa kwasababu nimeona nina uwezo huo,” amesema

Mbunge anayemaliza muda wake wa Jimbo hilo ni Bonnah Kamoli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mwili wa Hayati Mwinyi kuagwa leo saa 8 Uwanja wa Uhuru

Spread the loveMWILI wa Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi unatarajiwa kuagwa kuanza...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi kuzikwa Machi 2 visiwani Unguja

Spread the loveMWILI wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Tanzania,...

Habari za SiasaTangulizi

Rais mstaafu Mwinyi afariki dunia

Spread the loveRais Mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania, Ally Hassan...

Habari za Siasa

Waziri mkuu Ethiopia atua Tanzania

Spread the loveWaziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia,...

error: Content is protected !!