Monday , 26 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Agizo la Magufuli lawatafuna wafungwa Moro
Habari za SiasaTangulizi

Agizo la Magufuli lawatafuna wafungwa Moro

Moja ya Magereza yaliyopo mkoa wa Morogoro. Picha ndogo Rais wa Tanzania, John Magufuli
Spread the love

AGIZO la Rais John  Magufuli kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kukata umeme popote hata katika taasisi ya serikali imesababisha Magereza 14 katika mkoa wa Morogoro kukatiwa umeme na kusababisha wafungwa kuishi katika giza tororo, anaandika Dany Tibason.

Kutokana na kukatiwa umeme kwa magereza hizo askari wanalazimika kutumia tochi, vibatali katika nyumba zao kutokana na wao pia kukatiwa umeme jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa askari magereza na wafungwa pia.

Devotha Minja, Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) alitoa kauli hiyo jana bungeni wakati akiuliza swali la nyongeza kwa kutaka kuelewa kama kitendo cha Magereza 14 katika mkoa wa Morogoro kukatiwa umeme kwa kutekeleza agizo la Rais la (KA-TA) kama siyo ukiukwaji wa haki za mfungwa ambazo serikali ya Tanzania ulisaini katika mkataba wa Umoja wa Mataifa.

Devotha amesema kutokana na kauli ya rais ya kuelekeza Tanesco kukata umeme katika taasisi mbalimbali sasa ni takribani mwezi mmoja katika Magereza 14 za Morogoro hazina umeme pamoja na nyumba za askari jambo ambalo linasababisha wafungwa hao kunyimwa haki zao za kuishi katika sehemu yenye mwanga wa kutosha.

Pia amesema maaskari magereza wanalazimika kutumia vibatali jambo ambalo ni hatari katika kulinda usalama wao pamoja na usalama wa wafungwa hao ambao kimsingi wanatakiwa kupata hiki yao ya kuishi katika eneo ambalo linaendana na mikataba ya haki ya mfuungwa ya umoja wa mataifa.

Akiendelea kuuliza maswali ya nyongeza, Devotha alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kukarabati au kujenga Magereza mapya au kuyapanua ili kuondokana na usumbufu mkubwa ambao wafungwa wanaupata kutokana na kuwepo kwa msongamano mkubwa gerezani.

Awali katika jibu la msingi la mbunge wa Viti Maalum, Zubeda Sakuru (Chadema) alitaka kujua serikali ina mkakati gani katika kufanya matengenezo na kulinda haki za wafungwa.

“Magereza mengi nchini hayo katika viwango na ubora na hivyo kuvunja haki za wafungwa, Je serikali ina mkakati gani katika kufanya matengenezo na kulinda haki za wafungwa,” alihoji Zubeda.

Akijibu maswali hayo Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwiguru Nchemba, alikiri kuwa magereza hizo hazima umeme kutokana na kauli ya KA-TA lakini suala hilo kwa sasa linashughulikiwa na malipo na ankra ya umeme italipwa.

Amesema taasisi nyingi za serikali ikiwemo magereza zimekumbana na adha ya kukatiwa umeme lakini hiyo ni kutokana na kufanya wahusika wa malipo kuwa makini na kuheshimu fedha za serikali kwa kutumia katika matumizi ambayo yamekusudiwa.

Akizungumzia ujenzi na upanizi wa magereza Mwigulu amesema kwa sasa wanajenga magereza kubwa katika maeneo ya kilimo na magereza zilizopo mijini zitakuwa kwa ajili ya mahabusu kwa nia ya kupunguza safari ndefu pindi wanapokuwa wakipelekwa mahakamani.

Akijibu swali la msingi Mwigulu amesema Jeshi la Magereza limekuwa katika kusimamia haki za wafungwa kwa kuzingatia sheria ya magereza No.34 ya Mwaka 1967  na kanuni za uendeshaji wa magereza za mwaka 1968.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Hamahama Ngorongoro kutikisa maandamano ya Chadema Arusha

Spread the loveMAELFU ya wanachama na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na...

Habari za SiasaTangulizi

Waliofariki ajalini Arusha kuagwa siku ya maandamano Chadema

Spread the loveMIILI ya watu 25 waliofariki dunia katika ajali iliyohusisha lori...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali kuiburuzwa mahakamani ajali iliyoua 25 Arusha

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), imeitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Samia atoa pole ajali iliyoua 25, kujeruhi 21 Arusha

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu...

error: Content is protected !!