June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Agizo la DC Kilosa lapuuzwa

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, John Henjewele (kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Utalii na Maliasili, Lazaro Nyalandu

Spread the love

MAUAJI kati ya wakulima na wafugaji wilayani Kilosa, Morogoro yanadaiwa kuchagizwa na utoaji rushwa kwa watendaji wa serikali na kisha kuruhusu mifugo kuingia. Anaandika Jimmy Mfuru … (endelea).

Mkuu wa wilaya hiyo, John Henjewele alipiga marufuku uingizwaji wa mifugo wilayani humo kutokana na maeneo ya kulisha mifugo kuwa machache lengo likiwa ni kupunguza migogoro kati ya wakulima na wafugaji.

Hayo yalibainika  wakati wa ziara ya waandishi wa habari kutembelea wilaya hiyo kuangalia namna wananchi wanavyonufaika na rasilimali za misitu.

Pia kuangalia changamoto zinazokabili mradi wa uzalishaji mkaa endelevu unaotekelezwa kwa pamoja na Shirika la Kuhifadhi misitu asilia Tanzania (TFCG), na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi Misitu Tanzania (MJUMITA). 

Mradi huo unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Uswis (SDC) ambapo unafanyika katika vijiji 10 katika  wilaya hiyo.

Aprili 27 mwaka huu wakazi wa Kijiji cha Kisanga kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali walizuia kundi la mifugo wapatao 550 iliyokuwa ikitokea Iringa na kuelekea kijiji jirani cha Zombo.

“Waliamua kuzuai kundi hilo la mifugo ambalo lilikuwa limefanya uharibifu mkubwa.kundi hilo lilikuwa la ng’ombe na mbuzi katika hali ya kutekeleza agizo la Mkuu wa Wilaya kukataza mifugo kuingia wilayani humo,” anasema Mtendaji wa Kijiji cha Kisanga, Ahmad Athman.

Athmnan amesema, baada ya kuwauliza wahusika waliokuwa na mifugo hiyo, walimwonesha vibali   vilivyoruhusu mifugo hiyo kuingia wilayani humo kutoka kwa Mtendaji wa Kijiji Cha Zombo, Adrian Kisani. Mifugo hilo ilikuwa mali ya Cplian Muhindi.

Akizungumzia tukio hilo Diwani wa Kata ya Kisanga, Hassan Kambenga alikiri kukamatwa kwa mifugo hiyo wakati ikiingizwa ambapo iliwalazimu kuwarudisha walikotoka ili kutekeleza kama agizo la Mkuu wa Wilaya hiyo lilivyoelekeza.

Kambenga amesema, uingizaji mifugo wilayani humo umekuwa changamoto katika misitu ya kijiji hicho hasa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uzalishaji wa mkaa endelevu kwa kuwa, mifugo hiyo imekuwa ikila machipukizi  ya miti inayoota baada ya kukatwa. 

“Wananchi kwa sasa wamekuwa wakinufaika na rasilimali zitokanazo na misitu kwa kuwa mapato yamekuwa yakibakia katika vijiji na kuelekezwa katika miradi ya maendeleo huku kujenga madarasa, maabara, nyumba za walimu na daktari,” amsesema. 

Mwenyekiti wa Kijiji cha Zombo ambacho mifugo hiyo ilikuwa inapelekwa, Boni Matayo amekana kuwa na taarifa taarifa zozote kuhusu mtendaji wake kutoa kibali cha kuingiza mifugo na kwamba, hakushirikishwa  kitu ambacho ni kinyume na maagizo ya ngazi za juu.

Mtendaji huyo Adrian Kisani alipopigiwa simu kuhusu suala hilo alikubali kutoa kibali hicho kwa Muhindi na kumuomba radhi mwenyekiti wake. Hata hivyo alikiri kupokea rushwa ya Sh. 15,000 na kudai alisahau agizo kutoka ngazi za juu.

Mkuu wa wilaya hiyo, John Henjewele alipoulizwa kwa nji ya simu ni hatua gani atakazomchukulia mtendaji huyo amesema, Dar es Salaam na kudai “waandishi hamruhusiwa kufanya kazi wilayani kwangu bila ruhusa yake. 

“Mwandishi yeyote haruhusiwi kuingia wilayani kwangu bila ruhusa yangu, lazima mwandishi aripoti kwangu kwanza ili nijue na niandae watu wa kuongea nae kule anakokwenda kutafuta habari.” Amesema Henjewele na kukata simu.

error: Content is protected !!