August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

AG Masaju ‘ambeba’ Magufuli

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Goerge Masaju akifafanua jambo.

Spread the love

HATIMAYE George Masaju, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), ameegemea katika kauli ya bosi wake, Rais John Magufuli inayokataza mikutano na maandamano nchini licha ya Katiba ya nchi kuruhusu, anaandika Pendo Omary.

Mbele ya waandishi wa habari leo, Masaju amekitaka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuheshimu katazo la vyombo vya dola kuhusu kusitisha “Oparesheni ya Umoja wa Kupambana na Udikiteta Tanzania (Ukuta).

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, AG, Masaju amesema anaaishangaa Chadema kutaka kupambanana na udikteta nchini wakati wakati hakuna udikiteta hapa nchini unaosemwa na chama hicho.

Chadema imepanga kufanya maandamano yasiyo na kikomo nchi nzima kuanzia tarehe 1 Septemba mwaka huu.

“Haya maandamano tayari yamekatazwa na vyombo vya dola. Lazima tuheshimu mahakama, Msajili wa vyama vya siasa, Tume ya Haki za Binadamu na Jeshi la Polisi.

“Mnatakiwa kufahamu kwanza matumizi ya neno Oparesheni ni makosa. Hili neno Oparesheni ni matumizi au hatua za kijeshi. Halafu maandamano hayo yanafanyika siku ya kuzaliwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania,” amesema.

Masaju ameongeza kuwa, maandamano na mikutano ya Chadema yamelenga kulidhalilisha jeshi la JWTZ ambalo linalinda amani na mipaka ya nchi huku akidai kuwa tarehe husika ni siku ya kupatwa kwa jua hivyo kutakuwa na watalii kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Masaju amesema, zuio la maandamano hayo linaloambatana na tamko la polisi la “hali ya usalama itakapotengamaa” linazuia majadiliano yoyote yanayotakiwa kufanyika.

“Unapozungumzia hali ya usalama Polisi hawawezi ku- negotiate (kujadiliana). Hilo litakuwa siyo jeshi,” amesema AG Masaju.

error: Content is protected !!