Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko AG atoa waraka kuwaonya Ma-DC, RC
Habari Mchanganyiko

AG atoa waraka kuwaonya Ma-DC, RC

Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Profesa Adelardus Kilangi
Spread the love

MWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG), Profesa Adelardus Kilangi, ametoa waraka kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya kukazia marufuku ya wateule hao wa Rais John Magufuli, kuwaweka watu mahabasu kinyume cha sheria. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa na Kepteni George Mkuchika, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora tarehe 15 Aprili 2019 bungeni jijini Dodoma, wakati akitoa ufafanuzi wa vitendo vya baadhi ya wakuu wa mikoa na wilaya kuwaweka watu mahabusu kwa saa 48 kinyume na sheria.

“Wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wanapotumia mamlaka yao ya kuweka mtu ndani saa 48 na 28 wazingatie sheria ya tawala za mikoa.

“Maelezo ya serikali kama nilivyoeleza huko nyuma ni kweli sheria ya tawala za mikoa na serikaliz a mitaa ya mwaka 97 inawapa mamlka wakuu wa mikoa na wilaya kumuweka mtu ndani pale inapothibitika anahatarisha amani.

“Naomba waheshimiwa wabunge msikilize hii sheria inavyosema, naomba mko waliko mnisikilize mtu anawekwa ndani kama amehatarisha amani, sio mtu anadaiwa madeni hataki kulipa unampeleka kwa mkuu wa wilaya anawekwa ndani, mtu asiwekwe mpaka amehatarisha amani.”

Mkuchika amesema, waraka huo unaeleza taratibu za wateule hao kumuweka mtu ndani, na kwamba kwa yeyote atakayekiuka matakw aya waraka huo, endapo akifunguliwa kesi binafsi kufuatia kitendo hicho, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali haitamtetea kwa kuwa amejitakiwa mwenyewe.

“Lakini nakushukuru sana mwanasheria mkuu wa serikali, sisi wengine tumeeleza kisiasa, mwanasheria wa serikali sasa ametoa waraka kwa wale wote waliopewa mamlaka ya kuweka mtu ndani.

“Kila mmoja ana barua ya mwanasheria mkuu wa serikali na mimi amenipa nakala, ninayo ikieleza ni mazingira yepi mtu anaweza kuwekwa ndani,” amesema na kuongeza;

“Moja ujiridhishe amefanya kosa la jinai, pili asubuhi uweke sababu kwa maandishi kwa nini umemuweka ndani, hawa watu wengi wanaowekwa ndani ni kauli tu ukimwambia hebu niandikie hataki, sheria inasema yawepo maandishi asubuhi yake apelekwe mahakamani, niwaombe wenzangu wenye madaraka hayo.”

Mkuchika amesema, mkuu wa mkoa na wilaya akitekeleza sheria kinyume na utaratibu anaweza kuchukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na yeye mwenyewe kushtakiwa binafsi.

“Mwanasheria wa serikali hatatetea mtu aliyevunja sheria makusudi kumuweka mtui ndani bila sababu, umetumia sheria vibaya utapelekwa mahakamani na huyo uliyemuweka ndani na mwanasheria wa serikali hatokuja kukutea,”amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa majina 12 ya familia moja waliofariki kwenye ajali Tanga

Spread the love  MAJINA 12 kati ya 17 ya waliofariki dunia katika...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awalilia 17 waliofariki ajalini wakisafirisha maiti

Spread the love  RAIS Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa...

Habari Mchanganyiko

Wanawake wachimbaji wajenga zahanati kuokoa afya za wakazi 2000

Spread the love  ZAIDI wakazi 2,000 wa kijiji cha Nyamishiga Kata ya...

Habari Mchanganyiko

Baada ya Congo DR, Somalia mbioni kujiunga na EAC

Spread the love  TAIFA la Somalia liko mbioni kuwa mwanachama rasmi wa...

error: Content is protected !!