March 3, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Afya ya Bulaya yaimarika Muhimbili

Spread the love

ESTHER Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), anaendelea na matibabu katika hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kufikishwa hospitalini hapo jana, anaandika Irene Emmanuel.

Akizungumza na MwanaHALISI Online, John Stephen, Ofisa Uhusiano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili amesema, Bulaya anaendelea na matibabu na hali yake ni nzuri.

“Esther Bulaya aliletwa hapa kwetu jana usiku saa tano, na alitokea hospitali ya wilaya ya Tarime, yuko hapa na anaendelea vizuri na matibabu lakini hatuwezi kuweka wazi nini kinamsumbua, ” alisema

Bulaya alikimbizwa hospitalini jana baada ya kuzidiwa na kupoteza fahamu akiwa rumande alikokuwa ameshikiliwa na jeshi la polisi Kanda Maalum ya Tarime akituhumiwa kuhutubia mkutano wa hadhara nje ya jimbo lake.

error: Content is protected !!