Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mama wa miaka 47 afungwa miaka 30 kwa kusafirisha dawa za kulevya
Habari Mchanganyiko

Mama wa miaka 47 afungwa miaka 30 kwa kusafirisha dawa za kulevya

Baadhi ya dawa za kulevya
Spread the love

 

LINNA Romani Maro (47), amehukumiwa kifungo cha miaka 30 gerezani na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, baada ya kukutwa na hatia ya kusafirisha madawa ya kulevya. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Katika Kesi ya jinai Na. 295/2018, Maro alitiwa hatiani baada ya mahakama kujiridhisha na ushahidi uliowasilishwa mbele yake na upande wa mashitaka.

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Agustina Mbando, ameeleza katika uamuzi wake aliyoutoa jana Jumanne, tarehe 2 Februari 2021 kuwa Linna ametiwa hatiani katika kosa la kusafirisha dawa hizo kinyume na kifungu cha 15 cha Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na madawa ya Kulevya Na. 5 ya mwaka 2015 sheria Na. 15 ya mwaka 2017.

Baro alifikishwa mahakamani baada ya kukamatwa na dawa hizo aina ya Heroin, zenye uzito wa gramu 43.95, mwaka 2018.

Kesi dhidi ya mtuhumiwa huyo, ilifunguliwa mahakamani hapo na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumatano na Afisa Mawasiliano wa DCEA, Daniel Kasokola, hukumu hiyo imetolewa jana tarehe 2 Februari 2021 na Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Agustina Mbando.

Mtuhumiwa huyo alikamatwa na DCEA tarehe 26 Januari 2018, maeneo ya Tabata Bima, wilayani Ilala,  mkoani Dar es Salaam.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

error: Content is protected !!