Tuesday , 21 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko AfrONet wapongeza uteuzi wa Dk. Mwatima.
Habari Mchanganyiko

AfrONet wapongeza uteuzi wa Dk. Mwatima.

Spread the love

 

MTANDAO wa Kilimo Hai Afrika (AfrONet), umempongeza Mwenyekiti wa Taasisi ya Kilimo Hai Tanzania (TOAM), Dk. Mwatima Juma kwa kuteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Baraza la Kumshauri Rais kuhusu Utekelezaji wa Masuala ya Kilimo na Chakula. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Rais Samia ameunda baraza hilo Machi 14, 2023, ikiwa ni kutekeleza azimio la viongozi wa Afrika, kupitia Mkutano wa Utoshelevu na Ustahimilivu wa Chakula (Dakar 2 Summit on Feed Africa, Food Sovereignty and Resillience) uliofanyika Dakar Senegal kuanzia tarehe 25 hadi 27 Januari 2023.

Mkutano huo ulihimiza kila nchi kuunda baraza la kusimamia utekelezaji mkakati wa kukuza kilimo na kuongeza uzalishaji wa chakula.

Pamoja na Dk. Mwatima wajumbe wengine Sekretarieti ni Katibu Mkuu mstaafu na Mwahadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Dk. Florence Turuka na Mkurugenzi Mtendaji wa Mazao ya Mbogamboga Tanzania (TAHA) Dk. Jacqueline Mkindi.

Kwa upande wa wajumbe wa Baraza hilo Rais Samia amemteua Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda ambaye ni Mwenyekiti, Mkurungenzi Mtendaji wa SAGCOT, Geoffrey Kirenga na Katibu Mkuu mstaafu Andrew Massawe.

Akizungumzia uteuzi huo Rais wa AfrONet Josephine Atangana, alisema mtandao huo unampongeza  Dk. Mwatima kwa kuaminiwa na Rais na matumaini yao ni kuona uwakilishi sahihi kwenye sekta ya kilimo na chakula.

Atangana amesema AfrONet ina matumaini makubwa kwa Dk. Mwatima na kuahidi kuwa watampa sapoti na ushirikiano wakati wowote katika majukumu mapya ambayo amepata.

“Uteuzi wako ni ushahidi tosha, kuhusu kazi zako kwenye mchango wako katika sekta ya kilimo hasa kilimo hai,” amesema,” Atangana.

Amesema Dk. Mwatima, ambaye ni Mwenyekiti wa TOAM wanatarajia atakuwa na mshauri wenye mwelekeo chanya katika kufanikisha malengo ya Dakar 2.

“Uteuzi huu tunaouona kwa mtazamo changa katika kuendeleza kilimo hai Tanzania na Afrika.

Akiwa kiongozi wa TOAM, Dk. Mwatima ameonesha dhahiri kuwajibika na kuelekeza katika kuhamasisha kilimo hai Tanzania hali ambayo imeboreha maisha ya wakulima.

Rais huyo wa AfrONet amesema Dk. Mwatima ana nafasi kubwa ya kufikisha sauti na mahitaji ya wadau wa kilimo hai kwa kuzingatia maazimio ya Dakar 2.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Tanzania yakabidhi rasmi msaada nchini Malawi

Spread the loveWAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,...

Habari Mchanganyiko

Bashe: Tumeshagawa pikipiki 5,500 kati ya 7,000 kwa maafisa ugani

Spread the love  WAZIRI wa Kilimo, Hussen Bashe, amesema wizara hiyo tayari...

Habari Mchanganyiko

Spika Tulia awapa neno mawaziri utekelezaji mashamba ya pamoja

Spread the love  SPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, amewataka mawaziri kushirikiana...

Habari Mchanganyiko

Ukosefu wa maadili kwa wakunga, wauguzi bado changamoto

Spread the loveIMEELEZWA kuwa vitendo vya uvunjifu wa maadili kwa  wauguzi na...

error: Content is protected !!