Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Afrika Kusini yataka mashirika kununua chanjo za Covid 19 Afrika
Kimataifa

Afrika Kusini yataka mashirika kununua chanjo za Covid 19 Afrika

Spread the love

 

RAIS wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa,ameyataka mashirika ya kimataifa na mashirika ya wafadhili kununua chanjo za Covid 19 kutoka kwa wazalishaji wa Kiafrika. Anaripoti Rhoda Kanuti kwa msaada wa Mashirika ya Kimataifa … (endelea).

Taarifa hiyo imekuja wakati mtengenezaji wa chanjo kutoka nchini Afrika Kusini, kutoa angalizo la kusimamisha uzalishaji wa chanjo hizo, kwa kukosa watu wanaoagiza.

Rais Ramaphosa ameyasema hayo, alipokuwa akizungumza katika mkutano wa kilele cha kimataifa kuhusu Covid 19 siku ya Alhamisi tarehe 12 mei 2022, kuwa hili ‘’nitahakikisha kuwa uwezo unaoendelea katika bara unadumishwa.’’

Akiongeza kuwa ‘’mashirika ya kimataifa ambayo yamechangiwa fedha nyingi kwa ajili ya kununua na kupata chanjo kwa nchi zilizoendelea kiuchumi ,hayanunui chanjo kutoka kwa watengenezaji wa chanjo barani Afrika,hata kwa zilie ambazo zimewekwa kwa nchi za Afrika,’’ alisema Ramaphosa.

Hata hivyo kampuni hiyo,ilijadili kutoa leseni mwezi Novemba ili kufunga na kuuza chanjo ya Johnson ili kusambazwa barani Afrika.

Aspen pharmacare hivi majuzi imesema kwamba, inaweza kulazimika kusitisha uzalishaji katika kiwanda chake cha Afrika Kusini, baada ya kukumbwa na uhitaji mdogo.

Aidha bara bado lina kiwango cha chini cha chanjo,hata wakati linakabiliwa na wimbi kubwa jipya la virusi hivyo.

Kati ya Waafrika sita, mmoja ndio amepata dozi za chanjo ya virusi vya corona,huku wengi wakisita kuchanja.

Ramaphosa alisema siku ya Alhamisi kuwa nchin yake bado inatetea msamaha wa haki miliki, ilikuboresha ufikiaji wa kimataifa wa chanjo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Ramaphosa akiri tatizo la umeme Afrika Kusini kuathiri sekta ya madini

Spread the love  RAIS wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amesema tatizo la...

Kimataifa

Idadi ya vifo tetemeko la ardhi yafikia 9000

Spread the love  IDADI ya vifo vilivyotokana na tetemeko la ardhi lililotokea...

Kimataifa

Tetemeko la ardhi Uturuki: Vifo vyaongezeka hadi 4,800

Spread the love  Idadi ya vifo vilivyotokana na tetemeko lililotokea jana Jumatatu...

Kimataifa

Tetemeko la ardhi laua watu 300 Uturuki, Syria

Spread the love  WATU  300 wamefariki dunia katika tetemeko kubwa la ardhi...

error: Content is protected !!