Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Afrika kusini waandamana kushinikiza serikali kumaliza tatizo la umeme
Kimataifa

Afrika kusini waandamana kushinikiza serikali kumaliza tatizo la umeme

Spread the love

 

MAMIA ya wafuasi wa Chama cha upinzani nchini Afrika Kusini – Democratic Alliance wameandamana jana tarehe 25 Januari 2023 kupinga kukatika kwa umeme kunakoendelea hali ambayo inazorotesha uchumi wa nchi hiyo iliyoendelea zaidi barani Afrika. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Afrika Kusini imeghubikwa na tatizo la nishati kwa zaidi ya muongo mmoja, lakini tatizo hilo limeongekeza zaidi mwaka huu, huku nchi hiyo ikikabiliwa na ukosefu wa umeme kila siku – wakati mwingine kwa muda wa saa 10 kwa siku.

Eskom – shirika la umeme la serikali lenye madeni, linakabiliwa na mitambo ya makaa ya mawe iliyochakaa ambayo inadaiwa kuharibika mara kwa mara.

Rushwa na hujuma pia zimelidhoofisha shirika hilo kwa kiasi kikubwa.

Kutokana na hali hiyo, Mkurugenzi Mtendaji, Andre de Ruyter wa shirika hilo anatarajiwa kuacha kazi mwishoni mwa Machi.

Mamia ya waandamanaji walikusanyika nje ya makao makuu ya chama tawala cha African National Congress, wakiilaumu serikali kwa kushindwa kutatua tatizo la umeme.

Mapema wiki hii, Rais Cyril Ramaphosa alisema serikali inaangalia suala la kuingiza umeme kutoka nje, lakini ameonya tatizo hilo haliwezi kutatuliwa kwa siku moja.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaKimataifa

Faye aahidi kuongoza kwa unyenyekevu, wagombea wenzie wakubali yaishe

Spread the loveMgombea wa upinzani Senegal, Bassirou Diomaye Faye anajiandaa kuwa rais...

error: Content is protected !!