Tuesday , 26 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Afrika kinara maambukizi ya homa ya ini, Serikali yahadharisha
Habari Mchanganyiko

Afrika kinara maambukizi ya homa ya ini, Serikali yahadharisha

Spread the love

WAKATI bara la Afrika likiwa kinara kwenye maambukizi ya ugonjwa wa homa ya ini duniani, Serikali ya Tanzania  imetoa tahadhari juu ya maambukizi ya ugonjwa huo pamoja na kuweka mkakati wa kuutokomeza ifikapo mwaka 2030. Anaripoti Faki Ubwa … (endelea).

Hatua hiyo imekuja baada ya takwimu za maambukizi ya ugonjwa huo iliyofanywa na Shirika la Afya Dunia (WHO) zinaonyesha kuwa mwaka 2019 watu milioni 296 walikuwa wanaishi na homa sugu ya ini ambapo asilimia 66 za waathirika walikuwa ni waafrika.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya ugonjwa hu oleo tarehe 28 Julai, 2022 jijini Dar es Salaam, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema tayari Tanzania imechukua hatua za kupambana na ugonjwa.

Waziri Ummy amesema siku hii ni ya kuelimisha na kukumbushana athari za ugonjwa huo .

“Leo ni siku maadhimisho ya homa ya ini duniani. Lengo kuu la maadhimisho haya ni kuielimisha na kuikumbusha jamii katika kutambua athari za ugonjwa wa homa ya ini” amesema Waziri Ummy.

Amesema asilimia za maambukizi ya ugonjwa huo kidunia zinachagiza serikali kutekeleza mpango wake wa kutokomeza  ugonjwa huo nchini  kufikia mwaka 2030.

“Hatua zinazofanywa na Wizara katika kudhibiti homa ya ini ni pamoja Kusimamia Mpango Mkakati wa Taifa wa Kudhibiti na Kutomeza Ugonjwa wa Homa ya Ini nchini wa mwaka 2018-2023”.

“Watu wapatao milioni 58 walikua wanaishi na maambukizi ya homa sugu ya ini aina ya C. Wakati huo huo kulikuwa na vifo 820,00 duniani kutokana na homa ya ini aina B duniani.

“Kwa Tanzania, takwimu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS) zinaonesha kuwa maambukizi ya homa ya ini aina ya B miongoni mwa wachangiaji damu kwa miaka mitatu ni kama ifuatavyo mwaka 2018 (4.4%), mwaka 2019 (5.9), mwaka 2020 (6.1%) na mwaka 2021 (5.3%). Aidha, kwa kipindi hicho maambukizi ya Homa ya Ini aina C yameendelea kuwa ni ya 2.3%” amesema Waziri Ummy.

Amezitaja sababu za maambukizi ya ugonjwa huo amesema kuwa ni pamoja  ngono kama  ambavyo Ukimwi  unaambukizwa.

Ametanabaisha aina nyingine ya ugonjwa huo ni ‘A’ na ‘E’ zinaambukizwa kwa njia ya maji yasiyokuwa salama yaliyochanganyika na kinyesi chenye virusi hivyo.

Waziri Ummy amesisitiza jitihada za serikali za kuutokomeza ugonjwa huo ni pamoja na kutoa elimu kwa wananchi, kuunganisha huduma ya homa ya ini na mpango wa taifa wa kudhibiti UKIMWI nchini, ili iwe rahisi kuwekea mikakati ya kudhibiti ugonjwa huu kwa kuhitimisha na utaratibu wa kuwapatia mama wajawazito kinga ya kuzuia maambukizi ya homa ya ini aina B kutoka kwa mama mjamzito kwenda kwa mtoto zipo katika hatua za mwisho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Rais Samia apewa tano ujenzi barabara Mtwara

Spread the loveWANANCHI wa Mkoa wa Mtwara, wameishukuru Serikali ya Rais Dk....

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kununua mitambo 15 ya kuchoronga miamba

Spread the loveSerikali kupitia Wizara ya Madini imepanga kununua mitambo 15 ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Mtanzania aweka rekodi kimataifa kwa kiwanda cha kusafisha dhahabu

Spread the loveIMEELEZWA kuwa Kiwanda cha Kusafisha dhahabu cha Geita Gold Refinery...

Habari Mchanganyiko

MAIPAC kusaidia Kompyuta shule ya Arusha Alliance

Spread the loveTaasisi ya Wanahabari ya kusaidia Jamii za pembezoni (MAIPAC) imeahidi...

error: Content is protected !!