June 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

AFP chafungua milango ya urais

Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chama cha Wakulima Tanzania (AFP), Mwarami Uwesu. Kulia ni Mkurugenzi wa Haki na Sheria, Abdul Ngakolwa

Spread the love

CHAMA cha Alliance For Tanzania Farmers Party (AFP), kimefungua milango kwa wanachama wake wanaotaka kuwania urais wa Tanzania katika uchaguzi wa Oktoba mwaka huu. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Gharama za fomu kwa nafasi ya urais ni Sh. 50,000, ubunge Sh.10,000 na udiwani Sh. 5,000.

Kwa Tanzania Bara, fomu zimeanza kutolewa Juni 15 mwaka huu, na tarehe ya mwisho ya kuzirudisha ni Juni 30 mwaka huu wakati Zanzibar wamechuku tangu Mei 15 hadi Juni 30.

Mkurugenzi wa Habari na Uenezi Taifa wa AFP, Mwarami Uwesu, amewaambia waandishi wahabari kuwa, wamejipanga vizuri mwaka huu na wanatarajia kumsimamisha mgombea urais, ambapo hadi sasa ameshajitokeza mgombea mmoja Zanzibar.

“Tumetoa gharama nafuu za fomu ili kuwapa moyo watu wengi kuchukua, hususani wanawake, hivyo tunaomba wanachama wajitokeze kwa wingi” amesema Uwesu.

Uwesu pia amezungumzia kuhusu maamuzi yaliyotolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Francis Mutungi ya kumrudisha katika uongozi Katiba Mkuu wa AFP, Rashidi Mrai, baada ya kusimamishwa na chama.

Kwa mujibu wa Uwesu, Mrai alisimamishwa uongozi kutokana na kutotimiza wajibu wake kulingana na matakwa ya chama.

“Sasa tumeshangazwa sana, Jaji Mutungi kuchukua maamuzi ya kumrudisha kwenye uongozi mtu ambaye amesimamishwa na chama. Sisi kama chama hatujaridhishwa na maamuzi hayo wala hatukubali ni lazima sheria ziheshimike,”amesema.

Ameeleza, “kitendo alichofanya Jaji Mutungi ni kuvunja katiba ya chama chetu, Ibara ya 10.A (3),…tunaomba afuate sheria na kuziheshimu.”

error: Content is protected !!