Saturday , 30 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Afisa wa serikali apora sanduku la kura Kinondoni
Habari za SiasaTangulizi

Afisa wa serikali apora sanduku la kura Kinondoni

Salum Mwalimu, Mgombea Ubunge KInondoni (Chadema) akihoji uchaguzi kuendelea baada ya sanduku la kura kuibwa na kurudishwa kituoni
Spread the love

AFISA mmoja mwandamizi wa serikali amepora sanduku la kupigia kura na kutoweka nalo, kwenye eneo la Magomeni, mtaa wa Idrisa, jimbo la Kinondoni, jijini Dar es Salaam. Anaripoti Faki Sosi…(endelea).

Taarifa kutoka eneo hilo zinasema, afisa huyo alitenda uharamia huo, katika kituo Na. 6 kilichopo kwenye eneo hilo.

Msafiri Salumu, wakala wa Chadema kwenye kituo cha Magomeni kwa Idrissa, anasema, katika kituo chake, “kuna gari limepaki pembeni. Mara akashuka jamaa mmoja, kama vile anataka kupiga kura, lakini ghafla akachukuaa sanduku. Akaondoka nalo.”

Anasema, “askari walikuwapo hapa, lakini hawakuchukua hatua zozote. Msimamizi wa kituo hiki Na. 6 anajibu kwa kiburi balaa. Sanduku limerejeshwa na anaruhusu watu kuendelea kupigakura kama kawaida.”

Uchaguzi mdogo kwenye jimbo la Kinondoni, unafanyika kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Maulid Said Mtulia, kwa maelezo kuwa anamuunga mkono Rais John Pombe Magufuli.

Mtulia alichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo, katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, kupitia Chama cha Wananchi (CUF).

Mgombea ubunge wa jimbo hili, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amesema, alifika kwenye kituo hicho baada ya kujulishwa kuwapo kwa tukio hilo.

“Nimefika kwenye kituo hicho na kuongea na msimamiza wa uchaguzi wa kituo hiki. Amekiri kuibiwa kwa sanduku hilo mbele ya askari wa jeshi la polisi. Hata afisa mkuu wa (mfawidhi) wa kituo hiki cha polisi naye amekiiri kutokea kwa kitendo hicho,” ameeleza Salum kwa njia ya masikitiko.

Kwa mujibu wa wakala huyo wa Chadema, aliyebeba sanduku hilo anamfahamu kwa kuwa ndiye aliyewaapisha kwenye ofisi za mtendaji kata.

Anasema, “huyu bwana aliingia hapa kituoni akiwa na askari wawili na kisha kuondoka na sanduku moja la kupigia kura lenye Na. 169624.”

Anasema, mtendaji huyo amefika hapo akiiwa na gari nyeupe aiana ya Toyota Rand Cruiser yenye rangi nyeupe na baadaye sanduku hilo lilirejeshwa kwa kutumia gari la polisi.

Msimamizi wa kituo hicho alipofuatwa na mwandishi wa kituo cha televisheni cha ITV ili kutoa ufafanuzi juu ya kilichotokea, aligoma kuzungumza kwa amdai ya kuwa hana mamlaka ya kufanya hivyo.

Hamisi Tutu mmoja wa wapiga kura kwenye kituo hicho amesema, anamfahamu aliyechukua sanduku hilo kwa kuwa ni mtumishi wa serikali anayewahudumia kwenye serikali ya mtaa wa Magomeni.

Nako kwenye kata ya Kigogo, wakala wa upinzani wamempiga msimamizi wa uchaguzi kwenye kata hiyo, baada ya msimamizi huyo msaidizi wa kituo hicho kuwatoa nje baadhi ya mawakala hao.

Taarifa zinasema, mawakala kadhaa wa Chadema wamezuiliwa kuingia kwenye vituo vya kupiga kura kwa madai kuwa hati za viapo vyao vilivyotolewa na msimamizi wa uchaguzi, ni batili.

Mgombea Ubunge wa Jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema, Mwalim amekamatwa na polisi baada ya kutaka uchaguzi katika kituo hicho usimamishwe kutokana na kutokea na hitilafu hiyo.

MwanaHALISI Online itaendelea kukuripoti matukio yote muhimu ya uchaguzi huu – Mhariri.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Gari la Mbunge Ole Sendeka lashambuliwa kwa risasi

Spread the loveGARI la mbunge wa Simanjiro (CCM) mkoani Manyara, Christopher Ole...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema: Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

error: Content is protected !!