April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Afisa Usalama wa Taifa feki akifikishwa kizimbani

Thomas Mgoli akiwa mahakamani

Spread the love

THOMAS Mgoli (37) amepandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kosa la kujifanya Ofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) na utakatishaji fedha. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Leo tarehe 20 Septemba 2019, mtuhumiwa huyo amesomewa mashtka matatu na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kelven Mhina.

Nchimbi amedai mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa alijifanya Ofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa kati ya tarehe 1 Agosti, 2019 na Agosti 2019.

Shtaka la pili, mtuhumiwa anadaiwa kujiingizia pesa kwa njia ya udanganyifu ambapo tarehe 17 Agosti 2019 na 29 Agosti 2019 alijipatia kiasi cha Sh. 280,500 kutoka kwa Lucy Ngongoseki akiwa eneo la Mahabusu ya Keko akijifanya Ofisa Usalama ambaye atamsaidia kwenye kesi namba 213 ya mwaka 2017 inayomkabili Jamal Malinzi aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Shtaka la tatu, mtuhumiwa anadaiwa kufanya utakatishaji fedha haramu katika tarehe 17 Agosti, 2019 na 29 Agosti 2019 alitumia pesa kiasi cha Sh. 280,500 ilhali akijua ni zao la kosa tangulizi la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Hakimu Mhina amesema kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo wala mamlaka ya kutoa dhamana upelelezi shauri hilo haujakamilika limeahilishwa hadi tarehe 4 Agosti, 2019.

error: Content is protected !!