Thursday , 28 March 2024
Home Kitengo Michezo Afisa Mtendaji mpya wa Simba aja na ahadi ‘bab kubwa’
Michezo

Afisa Mtendaji mpya wa Simba aja na ahadi ‘bab kubwa’

Senzo Mazingiza, Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba
Spread the love

KLABU ya Simba imemtangaza Senzo Mazingiza kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, akirithi mikoba ya Crescentius Magori, aliyemaliza muda wake, huku akitoa ahadi kede kede. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Akizungumza baada ya kutambulishwa, leo tarehe 7 Septemba 2019 jijini Dar es Salaam, Mazingiza ametaja maeneo matano atakayo anza kuyafanyia kazi kwa ajili ya kuipeleka Klabu ya Simba mbele.

Eneo la kwanza ni kubadili muundo wa uongozi, kwa kuhakikisha kwamba uongozi wa ndani wa Klabu ya Simba unakuwa huru na wa kitaaluma, wakati eneo la pili likiwa ni mabadiliko ya mfumo wa uchezaji.

“Kuna maeneo  ambayo nitaanza kuyafanyia kazi kwa ajili ya kufikia malengo tunayohitaji, eneo la kwanza ni muundo wa uongozi wa ndani, inatakiwa tuwe na muundo huru na wa kitaaluma kwa ajili ya kuipeleka klabu mbele. Pili, Simba ina klabu tanzu, ya vijana na wanawake, inatakiwa tubadili mfumo wa uchezaji,” amesema Mazingiza.

Eneo la tatu ni kuitangaza Klabu ya Simba kimataifa kwa kuanzisha kitengo maalumu kwa ajili ya kuitangaza klabu hiyo.

“Nataka kujielekeza kwenye utangazaji, tunahitaji kutambulika kimataifa, tunahitaji kuajiri watu wenye uzoefu na masuala ya masoko. Mfano miaka michache iliyopita nchini Uhispania klabu za mipira zilibadili mfumo wa masoko na kuzitangaza klabu zao nje ya mipaka yao. Ni muhimu na sisi kuonesha Simba si klabu ya Tanzania na Afrika Mashariki bali ni Klabu inayotambulika ulimwenguni kote,” ameeleza Mazingiza.

Eneo la nne ni uanzishaji miradi itakayowezesha klabu hiyo kuondokana na utegemezi wa misaada hadi kuwa klabu inayojiendesha kwa kutumia mapato yake ya ndani.

“Tunahitaji tuwe na mapato yetu, najua klabu nyingi za Tanzania na Afrika zinaendeshwa kwa njia mbili, michango na viingilio vya getini.  Tunahitaji kutafuta njia za kufanya biashara ili kupata fedha za kujiendesha na kulipa wachezaji,” amesema Mazingiza.

Mazingiza ameeleza kuwa, eneo la tano ni kutafuta mbinu za kuwabadilisha mashabiki kuwa wateja wa Simba kwa kuanzisha miradi ambayo mashabiki hao watakuwa wateja wakuu.

“Jambo la muhimu ni mabadiliko ya mashabiki kuwa wateja wa Simba. Tutaanzisha miradi ya kimkakati ambayo mashabiki watakua wateja,” amesema Mazingiza.

Mazingiza amesema chini ya uongozi wake atahakikisha Klabu ya Simba inatetea kombe la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara pamoja na kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa ikiwemo mashindano ya SportPesa, Kagame, Kombe la  Shirikisho na Ligi ya Klabu Bingwa Afrika.

Akielezea wasifu wa Mazingiza, Magori amesema alifanya kazi na Klabu ya Orlando Pirates, Platnum Stars FC, Chama cha Soka nchini Afrika Kusini na alikuwa miongoni mwa waangalizi wa michuano ya kombe la dunia iliyofanyika nchini humo mwaka 2010.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Makala & UchambuziMichezo

TFF kuamua hatima ya Amrouche

Spread the loveHATIMA ya Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche kuendelea...

Habari za SiasaMichezo

Matinyi: Dk. Ndumbaro alifanya utani ukaguzi mechi za Yanga, Simba

Spread the loveMsemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema kauli iliyotolewa na...

Michezo

Gethsemane Group Kinondoni (GGK) waachia video ya Bwana Wastahili

Spread the loveWAIMBAJI maarufu nchini kutoka Gethsemane Group Kinondoni (GGK)SDA wameachia video...

BiasharaMichezo

Gamondi kocha bora mwezi Februari, NBC yamjaza manoti

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!