April 15, 2021

Uhuru hauna Mipaka

AfDB yaikopa Tanzania Bil 414 kuipendezesha Dodoma

Spread the love

SERIKALI ya Tanzania imepewa mkopo wenye masharti nafuu wa zaidi ya Sh. 414 bilioni kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa barabara pamoja na uboreshaji miundombinu ya jiji la Dodoma. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Tarehe 19 Agosti 2019 Doto James, Katibu  Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Alex Mubiru, Meneja Mkazi wa AfDB walisaini makubaliano ya mikataba wa mkopo huo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya kusaini makubaliano hayo, James amesema benki hiyo itatoa dola 138 milioni na dola 42 zitatolewa na mshirika wake ambaye ni Mfuko wa Serikali ya China unaosimamiwa na AfDB.

James amesema, fedha hizo zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa barabara za mzunguko (barabara za pete) kwa kiwango cha lami umbali wa kilomita 110.2 kutoka Nala kwenda Veyula hadi Ihumwa mpaka Matumbulu.

Ameeleza kuwa, barabara hiyo ikikamilika itaungana na  barabara ya Cape hadi Cairo inayojulikana kama the Great North Road Highway yenye urefu wa Kilomita 10,228 inayopita katika nchi nane ambazo ni Afrika Kusini, Zimbabwe, Zambia, Tanzania, Kenya, Ethiopia, Sudan na Misri ambayo itaunganisha Tanzania na nchi za Jamhuri ta Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda na Uganda.

Pia, James amesema fedha hizo zitatumika katika uboreshaji wa miundombinu katika jiji hilo ikiwemo miundombinu ya huduma za kijamii ikiwemo maji na vituo vya afya, ukarabati w abarabara za michepuko sambamba na utekelezaji wa mikakati ta usalama wa barabarani katika mji wa Dodoma itakayotekelewa katika kipindi cha miaka mwili.

Kwa upande wake Mubiru amesema licha ya mikopo hiyo, benki ya AfDB inatarajia kutoa mikopo kwa ajili ya miradi mwili ikiwemo mradi wa uboreshaji barabara kutoka Bagamoyo kwenda Pangani  kisha Horohoro-Lunga-Mombasa- Mlaindi, nchini Kenya.

Mradi mwingine ni ujenzi wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Msalato. Mubiru amesema benki hiyo inatarajia kuipitisha miradi hiyo mwishoni mwa mwaka 2019.

error: Content is protected !!