MFANYABIASHARA ama mtoa huduma ambaye atabainika kuwepa kulipa kodi, akikamatwa atalazimika kulipa asilimia 100 ya kodi aliyotakiwa kulipa kama adhabu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Kwamba, kodi hiyo itakuwa mara mbili ya kodi anayodaiwa mteja, ambapo mapendekezo ya kuwekwa kwa adhabu hiyo yamefanywa na wabunge wa Bunge la Jamhuri.
Dk Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango akijibu hoja wakati wa kuhitimisha majadiliano ya Muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2021, amesema baada ya kusikia hoja za wabunge, serikali imeamua kuchukua ushauri kwa kuweka kifungu kipya cha kubana ukwepaji kodi.
Dk. Mwigulu amesema, makubaliano yaliyofikiwa katika kikao kati ya serikali na kamati ya bunge, ni kufanya mabadiliko kwenye tuliokuwa tumependekeza kuweka asilimia 75, wamependekeza kuwa asilimia 100 ya kodi iliyotakiwa kutozwa.
“Kwa maana hiyo, kodi itakuwa imezidishwa mara mbili ya iliyotakiwa kutozwa kama mtu huyo atakuwa amekwepa, kwa hiyo sisi kama serikali tunapokea maoni ya wa waheshimiwa wabunge na kamati ambayo ni mwakilishi wa Bunge,” amesema.
Leave a comment