Saturday , 13 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT-Wazalendo yatoa neno wanaokihama chama
Habari za SiasaTangulizi

ACT-Wazalendo yatoa neno wanaokihama chama

Spread the love

KATIBU wa Itikadi na mawasiliano ya umma wa Chama cha ACT-Wazalendo, Ado Shaibu amesema wimbi la wanachama wa chama hicho kuhamia CCM linakikomaza, anaandika Hamis Mguta.

Shaibu amesema hayo leo asubuhi katika mahojiano yake na kituo kimoja cha redio hapa nchini wakati  akizungumzia hali ya chama baada ya wimbi la wanachama wao kuendelea kuwakimbia.

“Siasa zinahitaji watu na viongozi makini, lakini tulishachora mstari baada ya kamati ya uongozi kukaa, Mwigamba na baadhi ya viongozi wana maoni ya kwamba tunakokwenda siyo sahihi na sisi wenyewe tunaamini kwamba tupo sahihi, ACT sasa ni chama cha kiaharakati,” amesema.

Amesema kuwa kama yupo mtu haridhiki juu ya msimamo wao  wa kupambana na serikali atoke. “Mtu akiondoka kwa sababu unapambana zaidi na serikali anakusaidia sana”

Amesema kuwa wanaowaza kuwa Zitto Kabwe yupo mbioni kuondoka katika chama hicho ni maono yao, lakini kama msemaji wa chama hana taarifa za Zitto kutaka kuondoka katika chama hiko na kurudi Chadema.

“Sijawahi kusikia mpango huo na sijawahi kuona kwa sababu mimi ndiyo msemaji wa chama na nashirikiu kuwepo kwenye vikao vyote na nafanya mawasiliano na viongozi wote,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Nchimbi aanika ugonjwa wa CCM

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Emanuel Nchimbi,...

Habari za Siasa

Chadema yapuliza kipyenga uchaguzi viongozi kanda

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeanza maandalizi ya uchaguzi...

Habari za Siasa

CCM :Hatutaki ushindi wa makandokando uchaguzi Serikali za mitaa

Spread the loveCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema hakihitaji ushindi wa makandokando katika...

Habari za Siasa

Makala: Puuzeni wanasiasa wanaojigamba wanaweza kubadili maamuzi ya mahakama

Spread the loveKATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),...

error: Content is protected !!