Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT-Wazalendo yataja mwarobaini ukali gharama za maisha
Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yataja mwarobaini ukali gharama za maisha

Spread the love

 

CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimeishauri Serikali iongeze shughuli za kiuchumi ili kukabiliana na changamoto za ongezeko la gharama za maisha, umasikini na ukosefu wa ajira. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ushauri huo umetolewa na Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, katika mahojiano yake na kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha ITV.

“Inapaswa ifanyike juhudi za makusudi kuongeza shughuli za kiuchumi, shughuli za uzalishaji hapa nchini na sekta ambayo inaweza kusaidia sana kuondokana na tatizo la ajira nchini ni sekta ya kilimo kuna kazi kubwa inapaswa kufanywa kuongeza shughuli za uzalishaji katika sekta ya kilimo, sio tu wazalishe lakini kuongeza thamani ya mazao,” amesema Zitto na kuongeza:

“Shughuli ya kilimo na mchakato wa kuongeza thamani ya mazao inaweza kutusaidia kukabiliana na matatizo matatu tunayokabiliana nayo, gharama ya maisha sababu sehemu kubwa ya gharama ni chakula ukiwa na cha kutosha unaukabili umasikini, ukishakuwa na shughuli za kiuchumi watu wanapata kipato na ukiwa na shughuli za kiuchumi unaajiri. Tunaishawishi Serikali itizame namna gani ya kupokea mtizamo huu ifanyie kazi ili kukabiliana na gharama za maisha na umasikini.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!