August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

ACT-Wazalendo yasema bei ya vyakula imepaa, yatoa mapendekezo

Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu

Spread the love

 

CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimedai gharama za maisha zimezidi kupanda huku hali ya uchumi wa wananchi ikiwa ngumu, hususan katika bei ya vyakula na bidhaa nyingine muhimu kama nishati ya mafuta. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo Alhamisi, tarehe 7 Julai 2022, jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu, akielezea waliyobaini katika ziara ya Sekretarieti ya chama hicho Taifa, katika kata za Jimbo la Mbagala.

“Kote tulikopita, kilio kikubwa cha wananchi ni hali ngumu ya maisha kunakotokana hasa na kupanda kwa bei ya bidhaa muhimu kama vile bidhaa za chakula, mafuta ya petroli na dizeli, bidhaa za ujenzi na nauli za usafiri wa daladala na za kwenda mikoani,” amesema Ado.

Katibu Mkuu huyo wa ACT-Wazalendo, amesema uchambuzi uliofanywa na chama chake katika ziara hiyo, umebaini bei ya vyakula muhimu kama mchele, unga wa mahindi, mafuta ya kupikia na maharage, imepanda ukilinganisha na kipindi kama hiki mwaka jana.

Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu, amesema ziara ya Sekretarieti ya chama hicho katika Jimbo la Mabagala, imebaini ongezeko la gharama za maisha na hali ngumu kiuchumi, ambapo amedai mchele umepanda kutoka Sh. 1,200 hadi 2,400. Unga (Sh. 1,000 hadi 2,400). Mafuta ya kupikia Sh. 3,000 hadi 9,000).

Ado amedai kuwa, katika ziara hiyo jimboni Mbagala na katika baadhi ya maeneo nchini, wameibaini bei ya mchele kwa kilo moja, imepanda kutoka Sh. 1,200 hadi 2,400, wakati unga wa mahindi ukipanda kutoka Sh. 1,000 hadi 1,600.

Bidhaa nyingine zilizopanda bei kwa kilo ni, unga wa ngano (Sh. 1,200 hadi 2,000). Sukari (Sh. 1,500 hadi 3,000). Nyama (Sh. 6,500 hadi 9,000) na mafuta ya kilo bei yake kwa lita moja imepanda kutoka Sh. 3,000 hadi 9,000.

Kufuatia changamoto hizo, Ado ametoa mapendekezo kadhaa kwa Serikali, ili yatekelezwe kwa ajili ya kupunga ukali wa gharama za maisha kwa wananchi, ikiwemo kutenga fedha za haraka kwa ajili ya kuongeza uwezo wa hifadhi ya mafuta ya petroli.

Katika hatua nyingine, Ado ameishauri Serikali kutengeneza mazingira mazuri yatakayowezesha wananchi kujiajiri, kama uboreshaji wa miundombinu ya masoko, kuwapanga wamachinga katika maeneo yenye mzunguko mkubwa wa watu.

Pamoja na wanaoendesha pikipiki za abiria, kuwekewa mazingira mazuri ya kutekeleza majukumu yao bila bughudha.

error: Content is protected !!