Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa ACT-Wazalendo yapata pigo Zanzibar
Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yapata pigo Zanzibar

Marehemu Habib Ali Mohamed
Spread the love

 

MWAKILISHI wa Jimbo la Mtambwe, visiwani Zanzibar, kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Habib Ali Mohamed, amefariki dunia, wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Saiffe, jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Habari, Uenezi, Mawasiliano na Umma ACT-Wazalendo,Salim Biman, Mohamed amefariki dunia alfajiri ya leo tarehe 3 Machi 2023.

“Chama cha ACT-Wazalendo kinatuma salamu za pole Kwa Spika wa Baraza la Wawakilishi, wananchi wa Mtambwe, ndugu, jamaa na marafiki wote wa marehemu Mohamed, kwa kuondokewa na kiongozi wetu, mwanafamilia na mpendwa wetu,” imesema taarifa ya Bimani.

Kupitia taarifa hiyo, Bimani amesema ratiba ya mazishi itatolewa baadae baada ya chama hicho kushauriana na famili ya marehemu Mohamed.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!