July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

ACT-Wazalendo yamtaka CAG afanye ukaguzi maalum fedha za muungano

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) nchini Tanzania, Charles Kichere

Spread the love

 

CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimeitaka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), afanye ukaguzi maalum kwenye mapato na matumizi ya fedha za muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ili kubaini kama zinagawiwa inavyostahili. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ushauri huo umetolewa leo Alhamisi, tarehe 16 Juni 2022, jijini Dar es Salaam na Msemaji wa Kisekta wa Fedha wa ACT-Wazalendo, Emmanuel Mvula, akichambua makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2022/23.

“Tunamshauri CAG afanye ukaguzi maalum wa fedha za muungano, mapato, matumizi na fedha zinazobaki ili kubainisha mgawo sahihi fedha ambazo Zanzibar inastahili,” amesema Mvula.

Katika hatua nyingine, Mvula amesema chama chake kinashauri Serikali ifanye upya utafiti wa mapato ya muungano huo, ili kupata takwimu sahihi.

Aidha, Mvula amesema chama chake kinashauri Serikali ianzishe akaunti ya pamoja ya fedha kwa mujibu wa sheria na mapato yote ya muungano yawekwe katika akaunti hiyo.

error: Content is protected !!