Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT-Wazalendo yalia rafu Z’bar
Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yalia rafu Z’bar

Nassor Ahmed Mazrui, Naibu Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo Zanzibar
Spread the love

CHAMA cha ACT-Wazalendo kimelaumu vitendo vya wagombea wao kuwekewa pingamizi ama kuondolewa na wasimamizi wa uchaguzi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Kimeeleza, iwapo hali ya uminyaji haki, uhuru na usawa inayoendelea visiwani Zanzibar kuelekea uchaguzi mkuu wa tarehe 27 na 28 Oktoba 2020 haitadhibitiwa, yapo madhara yanayoweza kutokea.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo Alhamisi tarehe 27 Agosti 2020, Nassor Ahmed Mazrui, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho visiwani Zanzibar amesema, chama hicho hakitakubali.

“Tumeanza kushuhudia mizengwe, njama na hujuma mbalimbali zinazofanywa na wasimamizi wa uchaguzi waliokosa maadili ya uchaguzi. Tunaomba tume iingilie kati,” amesema.

Amesema, kinachofanyika sasa ni wasimamizi wa uchaguzi visiwani humo kuwaengua wagombea wa baadhi ya vyama vya upinzani kwa kuwawekea pingamizi zisizokuwa na mantiki.

Maalim Seif Sharrif Hamad, Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo

Akitaja maeneo yaliyoingia kwenye mgogoro wakati wa uteuzi, miongoni mwao ni Wilaya ya Micheweni, Wilaya ya Mkoani, Wilaya ya Chake Chake, Jimbo la Chonga, Wilaya ya Wete.

“Wilaya ya Chake Chake, wagombea wa majimbo manne (Chake Chake, Ole, Wawi na Chonga) wamewekewa pingamizi. Wagombea wa Wilaya ya Chake Chake wamepingwa kwa kuambiwa hawana sifa za kugombea.

“Jimbo la Chonga, mgombea amebambikiziwa sababu ya kutokuwa na risiti ya malipo ya mahakama na Jimbo la Chake Chake, mgombea pia amebambikiziwa sababu ya pingamizi kuwa hakuwasilisha tume barua ya udhamini kutoka chama chake,” amesema Mazrui.

“Sisi tunasema amani ni pamoja na imani ambayo kwa sasa inaanza kufifilia na mwenendo huo. Kwa hivyo, hatunabudi kusema na kukiri bila ya haki hakuna amani! Sisi ACT Wazalendo tunaamini usemi huo kwani mahala isipotendwa haki na amani haiwezi kuishi.

“Tunainasihi Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuheshimu sheria, Katiba na Kanuni zilizopo na kamwe wasikubali kutumika kama mawakala wa kuitafutia CCM ushindi wa kupita bila kupingwa. Sisi hatutakubali..,” amesema.

Amesema, ni vyema NEC na mamlaka zote za kusimamia uchaguzi wakatambua bila kuwepo wagombea, hapatokuwa na uchaguzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!