Thursday , 18 April 2024
Home Habari Mchanganyiko ACT-Wazalendo yalia na uhaba wa walimu
Habari Mchanganyiko

ACT-Wazalendo yalia na uhaba wa walimu

Spread the love

CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimeishauri Serikali kuchukua hatua za haraka kupunguza changamoto ya uhaba wa walimu nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Ruvuma…(endelea).

Ushauri huo umetolewa leo Jumatatu na Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu, katika ziara yake mkoani Ruvuma, baada ya kutembelea Shule Shikizi ya Mwamko iliyoko Kata ya Mpepai, Jimbo la Mbinga, na kubaini ina mwalimu mmoja anayehudumia wafunzi 187.

“Tumefarijika na jitihada zilizochukuliwa kwenye ujenzi wa madarasa. Lakini, bado kuna uhaba mkubwa wa walimu. Mathalani, hapa Shule Shikizi ya Mwamko, kuna mwalimu mmoja tu anayefundisha Wanafunzi 187. Hili tunalichukua na tutalifikisha Serikalini”- amesema Ado.

Akiwa katika Shule ya Sekondari ya Ali Mohamed Shein, Ado amesema ziara yake hiyo ni utekelezaji wa falsafa ya ACT-Wazalendo ya “Siasa na Maendeleo”, ambayo inaelekeza wanachama na viongozi kutembelea miradi ya maendeleo.

“Mwaka 2018, Ndugu Zitto Kabwe alitembelea Kata zote zilizokuwa chini ya ACT Wazalendo. Chama kilichokua hatua, mbali na kuiwajibisha Serikali, kupunguza changamoto kwenye Sekta ya maji, afya, barabara na masoko. Leo tupo Mpepai. Tunawaahidi pia watu wa Mpepai kuwa changamoto zote tumezichukua na tutawashirikisha wadau kuzitatua,” amesema Ado.

Ado anaendelea na ziara kwenye majimbo yote ya Ruvuma ambapo leo anafanya vikao katika Majimbo ya Mbinga Mjini na Nyasa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

Habari Mchanganyiko

Serikali yatoa ajira watumishi 46,000, yatangaza utaratibu mpya kuajiri

Spread the loveSERIKALI imetangaza nafasi za ajira za watumishi wa umma 46,000...

error: Content is protected !!