Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa ACT Wazalendo yaja na ahadi ya “Taifa la Wote kwa Maslahi ya Wote”
Habari za Siasa

ACT Wazalendo yaja na ahadi ya “Taifa la Wote kwa Maslahi ya Wote”

Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo
Spread the love

CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimezindua ahadi yake kwa Watanzania, ya kujenga Taifa la wote kwa maslahi ya wote kufikia 2035 endapo kitapewa ridhaa ya kuongoza Serikali kupitia Uchaguzi Mkuu wa 2025. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Ahadi hiyo imezinduliwa Leo Jumamosi, tarehe 18 February 2023, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema chama chake kimekuja na ahadi hiyo baada ya kuona nchi inakosa sera inayojenga taifa linalogusa maslahi ya wote.

“Tunaomba ufumbe mboni ya macho yako uifikirie kesho yako ambayo wewe umetupa ACT-Wazalendo kama madereva wa kuendesha gari ya kukufikisha kesho, kwa kura yako tutashinda uchaguzi halali na tutatekeleza Ilani yetu mpaka 2035. Unaamka kwenye taifa lenye uchumi jumuishi linalozalisha ajira za kutosha, watu wanaweza kumudu gharama nafuu za maisha,” amesema Zitto.

Zitto amesema ACT-Wazalendo inawaahidi Watanzania katiba bora inayowezesha mifumo bora ya utoaji haki na inayodhibiti vitendo vya rushwa.

Mwanasiasa huyo amesema kuwa, ahadi ya ACT-Wazalendo kwa Watanzania ni kuhakikisha vipato vyao vinaongezeka mara tatu na upatikanaji wa elimu bora bila malipo, inayowezesha vijana kushindana vizuri katika soko la ajira.

Ahadi nyingine ni kutoa ajira za kutosha kwa vijana, kujenga miundombinu imara, upatikanaji wa makazi bora na nafuu kwa wananchi na kupunguza gharama za vifaa vya ujenzi.

Kuhusu sekta ya afya, Zitto amesema chama chake kinawaahidi Watanzania kupata huduma bora za afya kupitia bima ya afya kwa wote, kuimarisha kinga za mwili dhidi ya maradhi mbalimbali.

“Tutajenga taifa linalotoa huduma kwa uwekaji bima kwa wote, mafao ya uzeeni. Taifa ambalo kila mwananchi anapata huduma safi na salama na maji ya uhakika,” amesema Zitto.

Katika sekta ya michezo, Zitto amesema ACT-Wazalendo inawaahidi Watanzania kuimarisha sekta hiyo kwa kuhakikisha nchi inakuwa kinara wa michezo Afrika na inashiriki michuano ya kombe la Dunia ya 2034.

Amesema kuwa, ni kwa namna gani ACT-Wazalendo itatekeleza ahadi hiyo, itafahamika katika mikutano ya hadhara watakayozindua kesho Jumapili, Mbagala jijini Dar es Salaam.

“Namna gani tutatatua migogoro ya ardhi ili watu wawe na ardhi ya wote kwa maslahi ya wote, namna gani tunapigania demokrasia ya wote kwa maslahi ya wote, namna gani tutahakikisha tunapata katiba bora ambayo itaangalia maslahi ya Watanzania wote, namna Gani tutatatua tatizo la kupanda gharana za maisha hasa bei za vyakula, tutaeleza kwenye mikutano ya hadhara,” amesema Zitto.

Zitto amesema kuwa, ACT-Wazalendo, inakusudia kuwaunganisha Watanzania pamoja na kuondoa siasa zinazowagawa.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!