Saturday , 3 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa ACT Wazalendo yaanika madudu miradi ya ujenzi, moundombinu
Habari za Siasa

ACT Wazalendo yaanika madudu miradi ya ujenzi, moundombinu

Reli ya kisasa ya SGR
Spread the love

CHAMA cha ACT Wazalendo kimeeleza wasiwasi juu ya uelekeo wa Serikali na mjadala unaondelea Bunge kuhusu ushirikishwaji wa sekta binafsi kwenye ujenzi wa miundombinu ya reli na barabara. Anaripoti Faki Ubwa…(endelea).

Hayo yameelezwa leo tarehe 23 Mei 2023 jijini Dar es Salaam na Msemaji wa Sekta ya Miundombinu, Reli na Barabara wa ACT Wazalendo, Mhandisi Mohammed Mtambo wakati akichambua Bajeti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2023/24.

Alisema kwamba ubia unaopigiwa chapuo kama njia mbadala ya kugharamia ujenzi wa miundombinu ni njia ya kuupumbaza umma juu ya athari za mwelekeo huu.

“Ubia ni ghali zaidi kuliko mfumo unaotumika hivi sasa. Athari zingine ni kwamba  mtindo huu unakuja na tozo kwa watumiaji ili kupata faida zaidi,” alisema

Alifafanua kuwa mfumo huu wa ubia ni njia ya kuficha deni la Taifa kwa mfumo wa kihasibu ambao hautokuwa wazi.

“Hii ni mbinu fiche ya ubinafsishaji wa miundombinu ya kimkakati ambayo kwa kawaida haipaswi kuwa mali ya mtu au Kampuni ambayo itatengeneza matabaka katika matumizi au bughudha wakati wa matumizi yake”, alisema.

Katika Uchambuzi huo ametaja hoja saba zinazohitaji kutazamwa ili kuifanya bajeti ya ujenzi na uchukuzi kuakisi matarajio ya wananchi.

Amezitaja hoja hizo kuwa ni kucheleweshwa  kukamilika na kuongezeka kwa gharama ujenzi wa Reli ya SGR ambapo ameeleza kwamba mradi wa Reli ya Kisasa kipande cha Dar- Morogoro na Morogoro hadi Dodoma kimechelewa kwa zaidi ya miaka mitatu jambo lililosababisha Serikali kutumia gharama za ziada za Sh 25 bilioni.

Aidha, alifafanua kuhusu uwekezaji wa kusuasua na hasara katika uendeshaji na usimamizi wa Ndege za Shirika la ATCL.

_”Tangu kufufuliwa kwa Kampuni hii mwaka 2016 kuna changamoto katika uendeshaji, zikiwemo mzigo mkubwa wa madeni, kuharibika mara kwa mara kwa injini za ndege na gharama kubwa za uendeshaji,” alisema.

Ameitaka Serikali kuiondoa TGFA (Shirika la Ndege za Serikali) Ofisi ya Rais Ikulu.

Pia ametoa rai kwa serikali kufanya ukaguzi maalumu wa manunuzi ya ndege tangu zilipoanza kununuliwa mwaka 2016 na kufanyike mapitio ya mikataba yote ya manunuzi ya ndege.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

Habari za SiasaTangulizi

Zanzibar watangaza rasmi kuwa shamba la Razaba ni mali yao

Spread the love  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetangaza rasmi kwamba shamba...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi azindua Kamati ya Maridhiano Visiwani

Spread the love  RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Hussein...

error: Content is protected !!