Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT Wazalendo wazindua ACT KIGANJANI
Habari za SiasaTangulizi

ACT Wazalendo wazindua ACT KIGANJANI

Kiongozi wa chama kikuu cha Upinzani nchini Zimbabwe cha Citizen Coalition for Change (CCC), Nelson Chamisa ( wa pili kushoto) akimkabidhi mjane wa aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamadi, Aweina Sinani, kadi maalumu ya kisasa iliyopewa jina la Maalim Seif. Anayeshuhudia ni Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe (wa kwanza kushoto).
Spread the love

 

CHAMA cha ACT Wazalendo kimezindua mfumo wa usajili wa kisasa wa wanachama wa chama hicho uliopewa jina la ‘ACT Kiganjani’ wenye lengo la kutibu tatizo la makusanyo ya ada za wanachama. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumzia mfumo huo jana tarehe 28 Januari, 2022 Katibu Mkuu wa chama hicho, Ado Shaibu amesema mbali na mfumo huo mbali na kuwawezesha wanachama kupata kadi za kisasa pia utawawezesha kulipia uanachama wao kupitia simu zao za mkononi.

Akifafanua kwa kina dhumuni la uzinduzi wa mfumo huo, Shaibu amesema ACT Wazalendo kupitia msingi wake wa uwazi kimekuwa chama ambacho kwa miaka mingi mfululizo kina uhakika ya kupata hati safi kila kinapokaguliwa na Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG).

Amesema hata CAG au Msajili wa vyama akifika katika ofisi zao wamekuwa hawana wasiwasi wa kupata hati safi.

“Ila jambo moja dogo ambalo limekuwa likinitia dosari muda mrefu kwa uzoefu wangu kama afisa masuhuli wa chama na limekuwa likijirudia kwenye taarifa nyingi za CAG ni udhaifu wetu wa kukusanya ada za wanachama.

“Hivyo basi tunachozindua leo (jana) pamoja na mambo mengine kinaenda kutibu suala hili one and for all. Halitojitokeza tena,” amesema.

Amesema uzinduzi huo wa ACT Kiganjani unalenga kuziba udhaifu wao kama chama lakini kukaribisha chama karibu na wananchi kupita teknolojia.

“Sasa kila mwanachama atasajiliwa, atapatiwa kadi mpya ya kisasa na ataweza kulipia ada yake ya uanachama wake kila mwezi kupitia simu yake ya mkononi,” amesema.

Aidha, amesema kazi hiyo ya kutengeneza mfumo huo wa kisasa imesimamiwa na vijana wa chama hicho.

Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe (kushoto) akipokea kadi yake ya uanachama wa chama hicho kutoka kwa Kiongozi wa chama kikuu cha Upinzani nchini Zimbabwe cha Citizen Coalition for Change (CCC), Nelson Chamisa. Chamisa alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kadi hizo mpya za kisasa.

“Hili jambo linanipa fahari sana mimi kama katibu mkuu wenu pamoja na sisi viongozi wa chama kwa ujumla wetu.

“Kwamba mfumo wa ACT Kiganja ni ubunifu wa vijana wetu ndani ya chama, vijana hao wakiongozwa na idara ya Oganaizesheni, Katibu wa Oganaizesheni Shaweji Mketo, Naibu Katibu wa Oganaizesheni Omari Ali Shehe wakisaidiwa na msimamizi wa masuala ya kitaalamu ya mfumo huu, Seif Hassan.

“Wamefanya kazi usiku na mchana kuhakikisha hiki kinachozinduliwa kinatokea,” amesema.

Amesema ujio wa mfumo huo, uwe changamoto kwa vijana wote kwamba wanayo fursa ya kutumia vipaji vyao katika kukisaidia chama chao.

“Niwapongeze wote ambao tayari mmeshasajiliwa katika usajili wa majaribio, wapo waliojitokeza na wamekwishasajiliwa,” amesema.

Pamoja na mambo mengine mfumo huo utawawezesha wanachama wa chama hicho kununua kadi za uanachama kwa bei mbalimbali kwa lengo la kuchangia chama.

Kadi hizo zilizopewa majina maalumu na bei tofauti ni kadi ya Maalim Seif inayouzwa kwa thamani ya Sh 200,000, kadi ya Tanzanite sh 100,000, kadi ya karafuu Sh 10,000, kadi ya kawaida Sh 2000.

Mfumo huo sasa unapatikana katika simu rununu kwa kupakua program hiyo ya ACT Kiganjani kupitia App store.

Katika uzinduzi huo, mgeni rasmi alikuwa Kiongozi wa chama kikuu cha Upinzani nchini Zimbabwe cha Citizen Coalition for Change (CCC), Nelson Chamisa.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!