December 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

ACT-Wazalendo wapinga uteuzi wa Mkurugenzi wa ZEC

Ado Shaibu, Katibu Mkuu ACT-Wazalendo

Spread the love

 

CHAMA cha ACT-Wazalendo kupitia Ofisi ya Katibu Mkuu Taifa, kimeinga uteuzi wa Mkurugenzi mpya wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Thabit Idarous Faina, kwa madai kuwa ndiye aliyesimamia na kuratibu Uchaguzi wa mwaka 2020 uliogubikwa na kasoro. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaa …(endelea).

Chama hicho kimetoa msimamo huo leo Ijumaa tarehe 11, Novemba, 2022 katika taarifa yake kwa umma, ikiwa ni siku moja tangu Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi kufanya uteuzi wa viongozi mbalimbali akiwemo Faina ambaye awali alikuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.

Taarifa hiyo imedai kuwa Faina ndiye aliyekuwa Mkurugenzi wa ZEC kwa kipindi cha mwaka 2017 hadi 2020, “kwa wadhifa huo ndiye aliyesimamia na kuendesha uchaguzi ulioleta fitina na maafa makubwa mwaka 2022.”

Taarifa hiyo imeendeela kudai kuwa Wazanzibar walishuhuidia kiwango kikubw acha kukosa uadilifu na kushindwa kutimiza wajibu wake wa kusimamia uchaguzi ulio huru na wa haki.

“Ni kwa mnasaba huo Wazanzibar na sisi ACT-Wazalendo hatukutarajia kabisa kuona kuwa ndugu Faina anarejeshwa tena kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi. Uteuzi huo unawafanya wapenda demokrasia na waumini wa maridhiano kutilia shaka dhamira ya Dk Mwinyi juu ya kupata maridhiano ya dhati.

“Sisi ACT-Wazalendo na wapigania demokrasia na maridhiano ya kweli tunamtaka Dk. Mwinyi atengue uteuzi wake haraka kabda ya umwapisha ili kujenga imani kuwa kweli amedhamiria kuleta maridhiano na utengamano w akweli hapa Zanzibar…” kimeeleza chama hicho.

error: Content is protected !!